Majeshi ya serikali ya Syria yameendelea kuwashambulia waasi
kwa mizinga katika mji wa Aleppo, kaskazini mwa Syria.
Pia
zimepatikana taarifa juu ya kutokea miripiko katika mji mkuu,
Damascus.
Wakati huo huo,Marekani na
Uturuki zinatafakari njia zote za
kuwasaidia waasi wanaopigana ili kuuangusha utawala wa Bashar
al-Assad.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton aliye ziarani
nchini Uturuki, amesema njia hizo ni pamoja na kuzipiga marufuku
ndege za majeshi ya serikali ya Syria kuruka katika maeneo fulani ya
anga.
Baada ya mazungumzo na waziri mwenzake wa Uturuki Ahmet
Davutoglu, Waziri Clinton aliwaambia waandishi wa habari mjini
Istanbul, kwamba Marekani na Uturuki zinahitaji kupanga mikakati ya
jinsi ya kuwasaidia waasi ili kukomesha mauaji nchini Syria.
No comments:
Post a Comment