Tuesday, August 14, 2012

Boti ya wakimbizi yahofiwa kuzama Australia

Wasi umeongezeka juu ya hatima ya watu 67 wanaotafuta hifadhi, ambao boti iliyokuwa ikiwasafirisha kutoka Indonesia kwenda Australia haijulikani ilipo kwa zaidi ya mwezi mmoja. 
Maafisa wa Australia wamesema leo kuwa kunna uwezekano kwamba boti hiyo ilizama. Waziri wa mambo ya ndani wa Australia Jason Clare amesema boti hiyo iling'oa nanga kwenye pwani ya Indonesia mwishoni mwa mwezi Juni au mwanzoni mwa Julai, na tangu wakati huo haijaonekana tena. 

 Tangu mwaka 2001, watu takribani 1000 wamezama baharini wakijaribu kwenda Australia kwa kutumia vyombo vya majini vya Indonesia visivyo na usalama wa kuaminika. 
Waziri mkuu wa nchi hiyo Julia Gillard amekwenda kufungua tena vitua vya wakimbizi kwenye visiwa vya Nauru na Papua New Guinea.

No comments:

Post a Comment