Tuesday, August 14, 2012

Wafanyakazi 4000 wa google kupoteza ajira

Kampuni ya mtandao wa internet Google imesema itafuta kazi zipatazo 4000 kwenye kampuni ya simu, Motorola Mobility.
 Google ambayo inaongoza kwa utafiti kupitia mtandao mwaka jana ilinunua kampuni hiyo yenye kuandamwa na hasara, kwa gharama ya dola bilioni 12.5. Imesema kufuta kazi hizo ni muhimu katika juhudi za kuifanya kampuni hiyo kuanza kupata faida tena, kwa kutengeneza zaidi simu za kisasa kuliko simu za kawaida.

Inaarifiwa kuwa asilimia 20 ya wafanyakazi wa kampuni hiyo watapoteza ajira, theluthi ya hao wakiwa nchini Marekani.
Watu wapatao 4000 wanatazamiwa kupoteza kazi zao kutokana na mpango huo.

No comments:

Post a Comment