Jeshi la Uganda limesema kuwa
helikopta zake nne zilizokuwa zimetoweka zikiwa njiani kuelekea nchini
Somalia sasa zimepatikana na abiria wote waliokuwa ndani yake wako
salama.
Akizungumza na BBC msemaji wa jeshi hilo Kanali Felix Kulaigye hakuweza kusema ndege hizo ziko wapi kwa sasa.Naye msemaji wa jeshi la Kenya, (Bogita Ongeri) ameiambia BBC kwamba operesheni ya kutafuta ndege hizo ilikuwa imevurugwa na hali mbaya ya hewa na kuongeza kuwa helikopta hizo nne zilikuwa kwenye safari hiyo kutoka nchini Uganda.
Moja ya helikopta hizo ilitua katika mji wa Garissa. Rubani aliyekuwa kwenye helikopta ya pili alizungumza na mamlaka za kenya akisema yuko katika eneo la mlima kenya lakini hakukukuwa na mawasiliano na helikopta nyingine mbili.
Helikopta hizo za Uganda hutumiwa kusindikiza misafara kutoka angani, katika opereresheni za utafutaji na uokoaji pamoja na kushambulia wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabaab nchini Somalia.
HELKOPATA HIZO
Helikopta tatu za Uganda zikiwa njiani kuelekea Somalia
zimepotea katika ardhi ya Kenya. Maafisa wa jeshi la Kenya wamesema leo
kwamba helikopta nne ziliondoka Uganda na moja ikatuwa mjini Garissa.
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Kenya Bogita Ongeri, helikopta hizo
zilipotea karibu na eneo la mlima Kenya, lakini rubani mmoja aliweza
kuwasiliana nao, akiomba msaada.Kwa mujibu wa msemaji huyo, mvua na
hali mbaya ya hewa zilihujumu juhudi za uokozi na Ongeri akaongeza
kwamba kundi la waokowaji limepelekwa sehemu hiyo ya ajali. Hata hivyo
alisema hawafahamu kwa uhakika ni wapi hasa ajali hiyo ilitokea kwa
sababu bado hali ya hewa ni mbaya. Helikopta hizo aina ya Mi-24
zinauwezo wa kubeba hadi abiria wanane.Helikopta hizo ambazo ziliondoka Uganda jana, zinahofiwa kuwa zimeanguka kwenye eneo moja la milima lililojaa misitu, karibu na mlima wenye theluji wa Kenya na ambao una urefu wa mita 5,199. Mkuu wa Polisi wa mkoa Francis Munyambu amesema taarifa walizonazo ni kwamba kuna mahala mahsusi ambapo inaaminiwa ndiko kulikotokea ajali hiyo.Aidha Mbali na helikopta za kivita M-24 Uganda inaripotiwa pia kupeleka Somali ndege za uchukuzi zilizotengenezwa Urusi aina ya Mi-17.
Umoja wa Afrika wapanga kushambulia Kismayu
Wanajeshi wa Umoja wa Afrika wamepelekwa Somalia
Wiki iliopita , Uganda ilitangazawa kwamba itatuma helikopta za
kivita nchini Somalia kukiimarisha kikosi cha wanajeshi 17,000 cha
Umoja wa Afrika kilichoko nchini humo kupambana na waasi wa Al-Shabaab
wenye mafungamano na Al-Qaeda.Akiwa ziarani nchini Uganda juma lililopita sehemu ya ziara yake ya siku 11 barani Afrika, Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton, aliipongeza nchi hiyo kwa mchango wake katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia.
Mbali na Uganda nchi nyengine zinazoshiriki katika kikosi hicho ni Burundi, huku Kenya na Djibuti zikisemekana pia kujiunga. Kenya iliingia vitani dhidi ya waasi wa Al-Shabaab ndani ya Somalia mwaka jana baada ya mashambulizi kadhaa ya kiagaidi nchini Kenya ambapo inaaminiwa yalifanywa na waasi hao.
Kikosi cha Umoja wa Afrika kinapanga masahambulizi makubwa katika mji wa kusini wa Kismayu, ambao ni ngome kuu ya Al-Shabaab, kabla ya Agosti 20. tarehe hiyo ndipo muda wa serikali ya sasa ya mpito utakapomalizika rasmi. Tayari bunge limepitisha katiba mpya ya muda na hatua hiyo itafuatwa na uchaguzi wa rais pamoja na kuundwa serikali mpya, itakayochukua nafasi ya utawala utakaoamalizika muda wake.
No comments:
Post a Comment