Wanamichezo watano waliohudhuria
miechezo ya Olympic jijini London Uingereza kutoka nchini Cameroon,
wanasema wanataka ukimbizi kuendelea kubaki nchi Uingereza baada ya
kutoweka katika kijiji cha Olympic wiki iliyopita.
Wanamichezo hao wanaume watano wote wakiwa ni
mabondia wameiambia BBC kuwa waliondoka katika kijiji cha mashindano ya
Olympic mashariki mwa London baada ya kutishiwa na maafisa wa juu wa
timu ya Olympic ya Camerron, kuwa wangeadhibiwa iwapo wangeshindwa
katika mashindano hayo.Akizungumza kwa niaba ya wenzake mmoja wa mabondia hao amesema wanataka kubaki nchini Uingereza ili kuendeleza taaluma yao ya kimichezo katika ndondi.
Hata hivyo mkuu wa msafara wa timu ya wanamichezo wa Cameroon David Ojong, amesema mabondia hao wamedanganya na kuwa hakuna yeyote aliyewatishia.
Amesema mabondia wote walipata mafunzo ya kutosha pamoja na kulipwa vizuri na sababu hiyo huenda ni kuhalalisha kurotoka kwao.
Mmoja wa mabondia hao Thomas Essomba amesema viongozi wa msafara wao waliwatisha kwa kuanza kuwaamuru wale waliokuwa tayari wameshiriki michezo mingine na kushindwa kusalimisha hati zao za kusafiria.
Naye bondia mwingine Blaise Yepmouo, amesema kamwe hawataki kurejea nchini mwao kwani taaluma yao ya kimichezo itakufa.
''Tunataka kuwa mabondia wa kulipwa na hatuwezi kurudi Camroon.'' Anasema. ''Na hata ikiwa tutarudi hatuwezi tena kuendelea na ngumi. Watano waliopo hapa wanataka kuwa mabondia wa kulipwa na ndiyo maana tunaomba udhamini.''
Wamesema kuwa kubaki kwao Uingereza kutawawezesha kupata udhamini na hivyo kuendeleza vipaji vyao katika mchezo huo.
No comments:
Post a Comment