Tuesday, August 21, 2012

Dala dala ya gongona na Noah jijini Arusha


Gari aina ya NOAH likiwa limeharibika vibaya baada ya kugongwa na Daladala alasiri ya leo Sanawari mkoani Arusha




DALADALA maarufu kama KIFODI inayofanya safari zake kati ya ARUSHA MJINI na NGULELO likiwa limeharibika vibaya baada ya kupata ajali mkoani ARUSHA


Ajali hiyo iliyotokea maeneo ya Sanawari jijini Arusha  ilihusisha magari manne ikiwemo NOAH ambayo imeharibika vibaya kwa upande wa nyuma wa gari hilo na magari mengine mawili ni VIFODI/daladala  vinavyofanya safari kutoka mjini kuelekea maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha

Chanzo cha ajali hiyo iliyotokea leo saa 3:15 alasiri ni mwendo kasi wa dereva wa Kifodi/daladala  kwa kutaka kuwahi mataa ya sanawari ndipo gari lilipomshinda na kugonga magari mengine.


Baada ya kutokea kwa tukio hilo dereva alitimua mbio kwa kuhofiwa kupigwa na abiria pamoja na wananchi wenye asira kali.

Abiria mmoja aliyekuwa na jazba ameeleza kuwa tangu" wametoka mianzini deleva alikuwa anaendesha gari rafu"  abiria huyo alifahamika kwa jina moja la Mwinshehe

Ajali hiyo haija jeruhi mtu yeyote zaidi ya magari yaliyo haribika na wote waliokuwa ndani ya daladala walitoka wazima.

UNA MAONI GANI KWA MADEREVA WANAO VUNJA SHERIA KWA MADAI YA KUWAHI TAA
habari na Mrisho S. Tozo wa arusha

No comments:

Post a Comment