Tuesday, August 21, 2012

Ikiwa Ni Miaka 7 Tangu Kifo Cha Vivian Na Comlex Hii Ndio Barua Kwa Vivian Toka Kwa Vijana Wa Hiphop Arusha (Sua)



Marehemu Vivian
Mpendwa Vivi,

Ni miaka saba sasa tangu uondoke na tunakukumbuka sana michano yako na mambo mengine mengi....(jalini ubinadamu msifanye mavitu kama sanamu.....). Natumai umeonana na Faza Nelly,DOG Nacko.Papaa,Mlost na Pacha Izzy na wengine wengi waliokuja huko.

Dhumuni la barua hii ni kukusalimu na kukujulisha yanayoendelea Arusha. Mengi yametokea ila ya Muhimu kukufahamisha kuhusu harakati za

Muziki hapa Arusha.
Imagine eti siku hizi Metropole,Ricks,Mawingu na Crystal club hazipo tena.Machizi wengi wamehamia Dar es salaam(just like you...) ila wao wamebadilisha hadi majina wanakuja Arusha kufanya show na kusepaz. Machalii wapya kibao kwenye Game na wanakalisha usipime wengine wako mbele na wanafanya harakati zilezile Kzz wa X plastaz hajarudi bado tangu aende na anatoa Mixtape moja kali sana hivi karibuni,Chindo pia anawakilisha akiwa huko si unajua tena Jamaa alivyo mbishi.
Jcb na Spark bado ni hardcore(...wana makid asee).maprodyuza wengi wapya na Studio nyingi.WATENGWA kuna Daz Naledge,DX amekuja na Noizmeka,hata Ngalimi siku izi kuna Studio asee KZ kaja na KAZAWAZA.Grandmaster siku izi wanapiga mpaka VIDEO bana.zipo mingi siwez hata kuzitaja zote.


Harakati zote zile za rap sasa hivi zimeamia Kijenge ya Juu(S.U.A Free-Stage).
Watu kibao wanakutana na kupiga freestyle,michano na magrafiit kibao.Si unakumbuka vile ulikua ukikasirika kuona hakuna mademu kwenye HIPHOP concert na ukawa unaamua kuonyesha uwezo wako dah! ulikua unakalisha asee(.....sa nani wakuongoza safari wote tunaujua usukani.......siwaelewi! )
Juzi si kuna madem wakaibuka SUA bana asee tulikukumbuka sana laiti ungekuwepo ungefarijika kinyama.

Kuna redio stesheni mingi niaje! karibu kila mtaa na maclub za kutosha huko town usiku kama tu mchana. ... kuna masista Dread wengi peace kama wewe.... inapendeza

Arif mambo kibao yamebadilika... kutoka TAPE na disc man siku izi kuna mavitu yanaitwa I-pod,I phone na ma-I pad kitu touch screen maamaaa si unajua Swagga tena...(sorry i know you now know about Apples kama sio matunda tena nikikuambia mambo ya Blackberry si ndo utadata kabisa...hahahahaha!!)

I will tell you about it next time sahivi naenda misele so kama vipi mpe hi Complex(Mwambie alivyosepa tu BTOWN CLAN wakaNYAMAZA ooh SH**T MIKOSI WAMENYAMAZA.....),James Dandu,Drob,Steve2k,produza Roy na wengine mlioko nao huko.

Jumapili tarehe 26 SUA itakua ni spesho kwako na Complex wa2 watapiga mistari yenu..oooyyyy! .Nitakujulisha zaidi next time.

Wako Wapendwa
Katika HIP HOP
###teamSUA###
KUTOKA KWA HAAZU NASEMA R.I.P VIVI, COMPLEX NA WOTE WALIOTANGULIA MBELE ZA HAKI WAKIWA NDANI YA ENTERTAINMENT INDUSTRY 
habari kwa hisani ya http/www. haazu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment