Tuesday, August 14, 2012

Dereva wa Bodaboda afa Mataa Chang'ombe jijini Dar es Salaam

Askari wa Doria ya pikipiki kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) akikagua ajali ya gari na piki piki iliyolihusisha Gari lenye namba T 871 BGY aina ya DCM Toyota linalofanya safari kutoka Temeke kwenda Mwenge likiwa limegongana na pikipiki namba T 107 BAK kwenye mataa ya Keko Chang'ombe. Ajali hii inasemekana imesababishwa na dereva pikipiki (ambaye alikufa hapohapo) kwani alipita wakati taa zikiwa zimeruhusu gari za kutoka Temeke zipite.

maoni ya mhariri wa sambweti.blogspot.com

kwa wale waendesha piki piki tukumbuke sisi ndio bodi/housing  ya piki piki kwa hiyo tunapokimbiana pik piki tukumbuke kujiwekea speed limit.

 kwa kutambua kuwa endapo ajali itatokea basi itakuhusu wewe pamoja na abiria ambaye umembeba na hata siku moja huwezi pata ajali mtu wa piki piki na fuso ukasikia dereva wa fuso amekufa kwa hiyo tuchukue tahadhari kwa maisha yetu wenyewe 

Picha: Rahel Pallangyo wa FK Blog.
  

habari kwa hisana ya  FATHER KIDEVU   blogu

No comments:

Post a Comment