kipimo cha CT Scan
Hatimaye kipimo
cha CT Scan cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kimetengamaa na
kuanza kutoa huduma kwa wagomjwa wanaoandikiwa kipimo hicho.
Akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana, Afisa Habari wa hospitali hiyo, Aminieli Eligaesha alisema kuwa kipimo hicho ambacho kiliharibika mwishoni mwa mwaka jana, kilianza kufanya kazi kuanzia Jumatatu ya wiki hii.
“Ni kweli kipimo cha CT Scan kilichokuwa kibovu kwa muda mrefu kimeanza kufanya kazi jumatatu, na kipo kwenye uwezo wake uleule wa kutoa huduma kwa wagonjwa,” alisema Eligaesha.
Kipimo hicho ni moja kati ya madai yaliyolalamikiwa na madaktari, ambao waligoma hivi karibuni wakiishinikiza serikali kuwawekea mazingira bora ya kazi.

Pamoja na kutaka mazingira mazuri ya kazi katika hospitali, madaktari hao pia waliitaka serikali kukitengeneza kipimo hicho ambacho walidai gharama zake haizidi bei ya gari moja linalotumiwa na mbunge.
Hata hivyo, akizumgumza hivi karibuni na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, Rais Jakaya Kikwete alikanusha kuwa bei ya kipimo hicho ni sawa na bei ya ‘shangingi’ moja, na kusema kuwa endapo kuna mtu anayejua kinapopatikana kwa bei hiyo basi na ampelekee.
No comments:
Post a Comment