Tuesday, August 14, 2012

Picha zaidi za tukio la kurejea kwa Dk Ulimboka


 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madakatari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka akiwa ameshika ua mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana, akitokea nchini Afrika Kusini kwa matibabu
  Wanaharakati wakipaza sauti wakati wa mapokezi ya Ulimboka.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madakatari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka akipata mapokezi makubwa wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo, akitokea nchini Afrika Kusini kwa matibabu baada ya kutekwa na kuteswa na watu wasiojulikana. Picha ya chini ikimuonesha Dk. Ulimboka akiwa katika hali mbaya baada ya kuokotwa katika msitu wa Mabwepande, Juni 27.
 Baadhi ya Wanaharakati pamoja na Madaktari wakilisukuma gari alilokuwa amepanda Dk Ulimboka mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment