Balozi wa Marekani nchini Libya na wafanyakazi wengine wa
ubalozi huo wameuawa kutokana na mashambulizi ya roketi katika mji wa
Benghazi yanayohusishwa na maandamano ya Waislamu kupinga filamu
inayomkashifu Mtume wao.
Waandamanaji hao walikuwa wamekasirishwa na filamu moja ya Hollywood ambayo inayakashifu kiongozi wa Waislamu, Mtume Muhammad. Maandamano kama hayo pia yalifanyika mjini Cairo, Misri, ambako maelfu ya waandamanaji waliuvamia ubalozi wa Marekani, lakini bila kuwapo visa vya mashambulizi. Wakristo wa madhehebu ya Koptik nao wamekusudia kufanya maandamano kupinga filamu hiyo, wakisema kuwa ni matusi kwa imani za watu wote.
No comments:
Post a Comment