Nakoula Basseley Nakoula a.k.a. Sam Bacile akiwa na mmoja wa wasanii wake Anna Gurji.
|
Tuesday, September 18, 2012 4:56 AM Wakati
maandamano ya kuipinga filamu ya kumashifu mtume (s.a.w) yakizidi
kupamba moto katika nchi mbalimbali duniani, mtengenezaji wa filamu hiyo
pamoja na familia yake ameingia mafichoni kunusuru maisha yake.
|
Nakoula
Basseley Nakoula, ambaye ni tapeli mwenye kujipa majina mbalimbali
mwenye umri wa miaka 55 ambaye alihukumiwa kwenda jela miezi 21 nchini
Marekani kwa makosa mbalimbali ya utapeli mwaka 2010, ameingia mafichoni
pamoja na familia yake baada ya maandamano ya kuipinga filamu
aliyoitengenza kuzidi kupamba moto.
Nakoula alijiita jina la Sam
Bacile wakati wa utengenezaji wa filamu ya "The Innocence of Muslims"
ambayo trela lake liliwekwa kwenye YouTube na video zake zikimuonyesha
mtu aliyeigiza kama mtume Muhammad, akifanya mapenzi, akibaka na
akiamuru kuuliwa kwa watu.
Nakoula aka Sam Bacile hajaonekana
tangu jumamosi baada ya polisi kwenda nyumbani kwake kumhoji na familia
yake ya watu wanne nayo jana jumatatu iliihama nyumba yao na kwenda
mafichoni kujiunga na Nakoula.
Polisi wa Los Angeles waliwasili
majira ya alfajiri kabla jua halijachomoza na walimchukua mke wa Nakoula
na watoto wake watatu na kuwasindikiza kwenye maficho ya siri ambako
Nakoula amejificha.
Familia yake ilizificha sura zao wakati
wakisindikwa na polisi toka kwenye nyumba yao iliyozungukwa na waandishi
wa habari wengi waliokuwa wakikesha mbele ya nyumba hiyo.
"Waliona
kuwa watakuwa salama sehemu ambayo wataweza kutoka nje na kuishi maisha
ya kawaida", alisema msemaji wa polisi na kuongeza "Tulichokifanya sisi
ni kuwachukua na kuwapeleka sehemu ambayo Nakoula amejificha".
Nakoula
aliwahi kutupwa jela miaka miwili iliyopita kutokana na utapeli wa
cheki za watu kwa kutumia majina mbalimbali feki. Alikaa jela mwaka
mmoja kabla ya kutolewa kwa masharti kumalizia kifungo chake uraiani.
Vyombo
vya habari vya Marekani vimekuwa vikiripoti kuwa kujihusisha kwake
kutengeneza filamu hiyo kunaweza kukawa kumevunja masharti aliyopewa
hivyo anaweza kurudishwa jela. |
No comments:
Post a Comment