Sunday, September 23, 2012

Maandamano ya Waislamu kuendelea weekend hii

Maandamano ya kupinga filamu inayoukashifu Uislamu yameendelea kufanyika katika sehemu mbalimbali duniani siku ya Jumamosi.
  Maelfu ya Waislamu waliingia mitaani siku ya Ijumaa katika mataifa ya Asia na Mashariki ya Kati kupinga filamu hiyo huku balozi za mataifa ya magharibi katika mataifa hayo zikifungwa kwa hofu ya vurugu.

Uchapishaji wiki hii wa vikaragosi vinavyomdhihaki Mtume Muhammad katika jarida la Charlie Hebdoe, la nchini Ufaransa, umezidi kuchochea hasira za waumini wa dini ya Kiislamu.


 Nchini Ujerumani, Waislamu wapatao 1,500 walifanya maandamano ya amani katika mji waDortmund jana. Ijumaa pia watu wapatao 1,000 walishiriki maandamano ya amani katika miji ya Freiburg na Muenster na maandamano mengine yanatarajiwa mwishoni  mwa juma  hili  katika miji ya Karlsruhe na Hanover.

No comments:

Post a Comment