Sunday, September 23, 2012

Wanamgambo Libya wavunja makundi yao

Makundi makuu mawili ya wanamgambo wa Kiislamu katika mji wa Derna, mashariki mwa Libya, na yanayofahamika kuwa  ngome ya Waislamu wenye msimamo mkali, yameondoka katika vituo vyake vitano siku ya Jumamosi, na kutangaza kuachana na shughuli zao.

 Hatua hizo za makundi ya Abu Salim na Ansar al-Sharia, zilichochewa na matukio ya mjini Beghazi ambako kundi la Ansar al-Sharia, linalohusishwa na vurugu za wiki iliyopita kwenye ofisi ya uwakilishi ya Marekani, liliondoka katika vituo vyake kufuatia maandamano makubwa ya kuiunga mkono serikali.

Shirika la habari la Libya LANA liliwanukuu makamanda wa makundi yote wakisema kuwa wanayavunja na kuondoka katika vituo vyao.

No comments:

Post a Comment