Mchezaji kiungo wa timu ya
Afrika Kusini,Thulani Serero huenda akakosa fainali za Kombe la Mataifa
ya Afrika za mwaka 2013 zitakazofanyika nchini Afrika Kusini kutokana na
maumivu ya nyonga aliyopata mwezi uliopita
"Hata kama atapona haraka, klabu pamoja na mcezaji mwenyewe, inabidi tuwe makini kuhusu hali yake."
Klabu ya Ajax imeongeza kuwa: "Thulani alikumbwa na majeraha madogo madogo msimu uliopita na sasa alikuwa mchezaji wa mara kwa mara kwa timu ya Ajax, kwa hiyo tatizo hili ni gumu kwake."
Kukosekana kwa Serero katika timu ya Bafana Bafana ni pigo kubwa kwa Afrika Kusini, hususan baada ya nahodha wa timu hiyo kutangaza hivi karibuni kwamba anastaafu soka la kimataifa.
Ina maana kwamba litakuwa pengo kubwa kuwakosa wachezaji viungo wawili wa kutegemewa na kutaathiri nafasi ya timu ya Bafana Bafana kushinda katika ardhi yake.
No comments:
Post a Comment