Thursday, November 29, 2012

Demokrasia yanawiri Somaliland



Kampeini za uchaguzi wa mitaa Somaliland
Uchaguzi wa mitaa unafanyika katika Jamhuri iliyojitangazia uhuru wake ya Somaliland , ambayo ilijitenga na Somalia zaidi ya mika ishirini iliyopi .
Uchaguzi huo haufanyiki katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo ambayo yana mzozo na jimbo jirani la Puntland.
Inaripotiwa kuwa watu wengi wamejitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo na kuna misururu mirefu nje ya vituo vya kupigia kura
Tangu ilipojitangazia uhuru wake kutoka kwa Somalia mwaka 1991, Somaliland imekuwa ikipata mafanikio taratibu , lakini thabiti kuelekea demokrasia.
Hadi uchaguzi huu, ni vyama vitatu vilivyo ruhusiwa kuendesha shughuli zake . Sasa mfumo umewekwa na vyama saba vinachuana katika uchaguzi wa mitaa .

Vitatu vitakavyopata kura nyingi zaidi katika maeneo yote ya Somaliland vitaendelea kushindana katika uchaguzi wa bunge . Somaliland ni moja ya maeneo machache ya Somalia yaliyo na amani yanayoweza kuendesha uchaguzi .
Huenda maeneo mengine mengi ya Somalia yakasubiri kwa miaka kadhaa kabla ya kuweza kutekeleza haki yao ya kupiga kura.

No comments:

Post a Comment