Tuesday, November 6, 2012

Mistari mirefu ya wapiga kura Marekani


Mjini Washington DC wapiga kura walipiga foleni masaa kadhaa kusubiri zamu yao. Shirika la habari la NBC limeripoti kwamba wapiga kura katika jimbo linalowaniwa vikali la Ohio walisubiri vituoni kwa zaidi ya saa nzima. Wakaazi wa jimbo la New Jersey lililoathiriwa vibaya na kimbunga Sandy wataweza kupiga kura kwa kutumia barua pepe au kwa njia ya fax.
 Katika jimbo jirani la New York ambalo pia lilipigwa na kimbunga hicho, raia wanaruhusiwa kupiga kura katika kituo chochote kile, bila kujali walikojiandikisha. Kura za maoni zimeonyesha wagombea wote wawili, Rais Barack Obama na mpinzani wake wake wa chama cha Republican Mitt Romney wakiwa sambamba, ingawa Obama alipewa nafasi ndogo ya kushinda.

No comments:

Post a Comment