Cameron amekiambia kituo cha televisheni cha al-Arabiya mjini Abu Dhabi, kwamba chochote kinaweza kufanywa kuhakikisha Assad anatoka nchini Syria, na kuruhusu kipindi salama cha mpito. Waziri Mkuu huyo wa Uingereza amesema hata hivyo angependa kumuona rais Assad akiwajibika kwa uhalifu alioutenda, lakini akaongeza kwamba iwapo anataka kutoka ndani ya Syria, mpango unaweza kufanywa kumsaidia.
Cameron amesema kwamba hakuna uwezekano wa Assad kupewa hifadhi nchini Uingereza. Haijulikani iwapo bwana Cameron alikuwa akitoa maoni ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, juu ya kumpa kinga rais Assad endapo ataamua kuhamia katika nchi nyingine.
No comments:
Post a Comment