Wednesday, November 21, 2012

Raia wa Ufaransa atekwa Nyara Mali




Wapiganaji wa waasi nchini Mali
Raia mmoja wa Ufaransa ametekwa nyara na watu wenye silaha Kusini Magharibi mwa Mali.
Alitekwa nyara siku ya Jumanne mjini Diema baada ya kuvuka na kuingia Mali akitokea Mauritania.
Ufaransa imethibitisha kuwa raia wake huyo ametekwa nyara nchini Mali.
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, amesema watafanya kila linalowezekana kukumpata raia huyo.
Kiongozi mwa wa kundi la Al-Tawhid na Al Jihad ambalo ni moja ya makundi katika vugu vugu la Movement for Oneness and
Jihad in West Africa, MUJAO anethibitisha kuwa kundi hilo lilitekekeza utekaji nyara huo.
Kiongozi huyo alisema baada ya mkutano wa dharuru na wanachama wa vugu vugu hilo katika eneo la Gao, raia huyo wa Ufaransa ametekwa nyara na wapiganaji wa Kiislamu maarufu kama Mujahidin na kuwa kundi hilo litatoa tangazo ramsi baadaye.
Wakati huo huo kundi la Ansar al-Din limekanusha kuhusika na operesheni iliyopelekea kutekwa kwa raia huyo wa Ufaransa Kaskazini mwa Mali.

No comments:

Post a Comment