Waangalizi kutoka Jumuiya ya Madola, ECOWAS na kikundi cha CODEO cha nchini Ghana walisema kuwa uchaguzi ulionekana kuwa wa amani na wenye uwazi, lakini Akufo Addo alisema jana kuwa hayuko tayari kukubali kushindwa. Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jay Carney alisema kwamba Mareni inawampongeza rais John Dramani Mahama na watu wa Ghana kwa uchaguzi wenye mafanikio wa tarehe 7 Desemba.
Alisema huu ni uchaguzi wa sita kuendeshwa kwa uwazi nchini Ghana tangu mwaka 1992, na ni ishara kwamba wananchi wa nchi hiyo wanajitolea kwa demokrasia na utawala wa sheria. Akufo Addo aliwaambia waandishi wa habari kwamba anaamini kulikuwa na udanganyifu katika uchaguzi huo uliofanyika Ijumaa iliyopita.
No comments:
Post a Comment