Amri yake hiyo imetolewa baada ya makabiliano baina ya wafuasi wa rais huyo na wapinzani wake wiki iliyopita, ambamo watu saba waliuawa na mamia kujeruhiwa. Chanzo cha ghasia hizo ni amri aliyoipitisha rais Mohammed Mursi tarehe 22 Novemba kujilimbikizia madaraka, na kuuweka uamuzi wake juu ya uwezo wa mahakama.
Kutokana na ghasia hizo, rais Mursi aliubatilisha uamuzi huo mwishoni mwa juma lililopita, lakini wapinzani wamesema hilo halitoshi. Mswada wa katiba utakaopigiwa kura ya maoni umekosolewa kuzikandamiza haki za raia na kuidhoofisha mahakama. Vyama vya upinzani vimeitisha maandamano makubwa leo Jumanne.
No comments:
Post a Comment