Tuesday, December 11, 2012

Rais aliamuru jeshi kudumisha amani


Vifaru vyadumisha amani
Vifaru vyadumisha amani
Rais Morsi wa Misri ameliamuru jeshi kudumisha amani na kuzilinda taasisi za serikali katika kipindi kinachotangulia kura ya maoni kuhusu katiba.
Viongozi wa upinzani wameshutumu kitendo hicho, na wameitisha maandamano yafanyike Jumanne.

Bwana Morsi amejaribu kutuliza maandamano ambayo yamekuwepo kwa siku kadhaa sasa, kwa kubatilisha amri iliyokuwa imempa mamlaka makubwa, lakini hata hivyo kura ya maoni ya 15 Desemba kuhusu katiba mpya bado itapigwa.Jon Leyne wa BBC, aliyeko mjini Cairo, anasema kwamba kitendo hicho kitakuza wasiwasi uliopo kwamba hali nchini Misri inarudi tena katika siku za uongozi wa kijeshi.
Maandamano
Vyama vya Kiisilamu vimesema kuwa nao pia wataandamana, jambo ambalo limezua wasiwasi kwamba makabiliano yanayotokea mara kwa mara katika barabara za mji mkuu wa Misri yatazidi kuwa makali.
Haijajulikana wazi kama upinzani utasusia kura hiyo ya maoni, mwandishi wetu anasema, ingawaje hali inaashiria kuwa wanaweza wakafanya hivyo.
Rais Mohammed Morsi
Rais Mohammed Morsi
Wanasema kwamba jopo lililorasimu katiba lilikuwa limejaa wapambe wa Morsi.
Katika taarifa iliyotolewa baada ya mazumgumzo ya Jumapili, chama cha National Salvation Front kilisema kisingetambua katiba rasimu "kwa sababu katiba hiyo haiwawakilishi wananchi wa Misri".
Kura ya maoni
Mnamo siku ya Jumapili, mamia ya wafuasi wa upinzani walikusanyika nje ya kasri la rais wakishtumu mpango wa kufanya kura hiyo ya maoni.
Huku wakiikashifu Muslim Brotherhood, waliimba barabarani na kubeba mabango yaliyosema "Morsi, wazuie majambazi wako" na "Wananchi wanataka serikali iondolewe ".
Amri hii mpya ya rais itaanza kutekelezwa mnamo siku ya Jumatatu. Jeshi limeombwa lifanye kazi pamoja na polisi ili kudumisha amani na usalama. Jeshi pia lina uwezo wa kuwakamata wananchi.
Jeshi limeshajenga ukuta wa saruji amabo umezingira kasri la rais, eneo ambalo wapinzani wanapenda kuandamana.

Amri
Waandamanaji nchini Misri
Waandamanaji nchini Misri
Rais anasema kwamba anajaribu kulinda mapinduzi yaliyompindua Hosni Mubarak mwaka uliopita, lakini wapinzani wake wanamnyooshea kidole cha lawama na kumuita dikteta.
Amri ya Bwana Morsi ya 22 Novemba iliinyang'nya mahakama haki ya kupinga maamuzi ya Morsi, na ikazua maandamano yaliyokuwa na vurugu.
Ingawaje amri hii imebatilishwa, maamuzi fulani yaliyochukuliwa awali yangali yapo.

No comments:

Post a Comment