Wednesday, February 27, 2013

PAMOJA NA BOMOA BOMOA KATIKA ENEO LA UBUNGO WAFANYA BIASHARA WAENDELEA NA BIASHARA


Baada ya kupita Bomoa Bomoa ya vibanda mbalimbali vya Biashara vilivyokuwa vimetapakaa na kujaza sehemu kubwa ya Stand Kuu ya Mabasi Ubungo (UBT) hali hivi sasa ndio kama inavyoonekana pichani.

Wafanya biashara wa maji, Juicena Vitu mbalimbali bado wapo na hivi sasa ni kwa staili ya Myavuli huku wakiwa wamepanga bidahaa zao katika vimeza na mbao.

Aidha bomoa boamoa hiyo pia imeathiria abiria ambao baadhi walikuwa wakitumia vibanda hivyo vya wafanya biashara kujisitiri kwa Juan a mvua wakati ama wakisubiri usafiri au kusubiri wageni wao kutoka mikoani.

hata hivyo leo majira ya saa kumi jioni magari mawili yakiwa na polisi waliojihami kwa silaha za mabomu ya macho za risasi za moto, walivamia eneo la Ubungo mataa kama unaelekea mwenge na kuwatwanya wafanyabiashara  na kuharibu baadhi ya vitu huku baadhi ya vijana wakikamatwa na kupelekwa kituoni.

cha kushangaza wakati tukio hilo linatokea eneo hilo la Ubungo mataa  baadhi ya wafanya biashara walitaharuki na kukimbia huku na huku , ili kunusuru bidhaa zao tofauti kabisa na wafanya biashara wadog  waliopo karibu  na stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani ambao walionekana wakiendelea na biashara bila bughaza yoyote.

No comments:

Post a Comment