TAHADHARI PICHA ZIFUATAZO ZINATISHA.
Hivi ndivyo anavyoonekana Majeruhi Yasin Rajabu na hapa akiwa amelazwa katika wod namba 8 Hospitali ya wilaya ya Geita kwaajili ya kupatiwa matibabu. |
Mwili wa marehemu mchungaji Mathayo Kachila ukiwa jokofu la mochwari kwenye hospitali ya wilaya ya geita. |
Hivi ndivyo anavyoonekana Majeruhi Said Ntahompagaze aliyejeruiwa mguu wakati wa vurugu za waislam na wakristu wachache zilizotokea leo katika kijiji cha Buseresere wilayani Chato mkoani Geita na kusababisha shughuli mbalimbali kusimama. |
Hivi ndivyo unavyoonekana mguu wa Said Ntahompagaze aliyejeruiwa wakati wa vurugu za waislam na wakristu wachache zilizotokea leo katika kijiji cha Buseresere wilayani Chato mkoani Geita na kusababisha shughuli mbalimbali kusimama. |
Majeruhi Vicent Damon akiwa amelazwa wod na 8 hospitali ya wilaya ya Geita aliyejeruiwa wakati wa vurugu za waislam na wakristu wachache zilizotokea leo katika kijiji cha Buseresere wilayani Chato mkoani Geita na kusababisha shughuli mbalimbali kusimama. |
Majeruh Sadick Yahaya. |
Majeruhi Ramadan aliyejeruiwa wakati wa vurugu za waislam na wakristu wachache zilizotokea leo katika kijiji cha Buseresere wilayani Chato mkoani Geita na kusababisha fukuto kubwa la vurugu zilizosababisha shughuli mbalimbali kusimama. |
Machafuko makubwa yametokea leo katika kijiji iislam kisha mwili wake kutelekezwa kwenye vibanda vya maduka ambavyo vilikuwa jirani na eneo hilo.
Habari za
kaminika eneo la tukio hilo lililotokea majira ya asubuhi zimeeleza kuwa
chanzo cha machafuko hayo ni watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wadini ya
kiislam kuvamia bucha lililokuwa likiwauzia nyama wakristo wa kijiji
hicho waliokuwa wamepanga foleni kwa wingi kusubili huduma hiyo.
Imeelezwa
kuwa Wakristu hao walikuwa wamechinjia ng'ombe mmoja na mbuzi wawili
eneo la Kanisani kabla ya kuleta nyama hiyo katika bucha hilo lililopo
eneo la Buselesele Sokoni na ndipo walipokumbana na kadhia hiyo ya
waislamu.
Tukio hilo
lilianza majira ya saa 2 asubuhi muda mfupi baada ya nyama kuwasili
katika bucha hilo la wakristu kwa ajili ya kuuzwa jambo linalodaiwa
liliwakera waislam ambao waliivamia bucha hiyo kwa lengo la kuifunga.
Wakati
wakristo wakitafakari uwepo wa waislam kwenye bucha lao lililpambwa kwa
maandishi BWANA YESU ASIFIWE, YESU NI BWANA, ndipo waislam ambao kwa
wakati huo walikuwa wametapakaa mtaani kwa lengo la kuhamasishana
waliongezeka eneo lilipo bucha hilo na kisha kuimwagia nyama iliyokuwa
kwenye bucha hilo vitu vinavyodaiwa kuwa ni sumu.
Kutokana
na hali hiyo wakiristo walionekana kukerwa na kitendo cha waislam
kuimwagia nyama hiyo vitu hivyo na kisha mapambano yalianza baina ya
wakristu na waislam ambapo mbali na wakristu kutumia mawe waislamu wao
walitumia mapanga na majambia.
Hata hivyo
wakati mapambano hayo yakiendelea mchungaji huyo ambaye kwa sasa ni
marehemu alifika eneo la tukio ili kujua kulikoni na ndipo naye
alipojikuta akishambuliwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za kichwa chake
na alifia njiani wakati akikimbizwa katika hospital ya Wilaya ya Geita
kwa matibabu zaidi.
Mbali na
mchungaji huyo kupoteza maisha,wengine waliojeruhiwa ni pamoja na Said
Ntahompagaze(45), Sadick Yahaya(40), Yasin Rajab(56), Vicent Damon(22),
wote wakazi wa Buselesele na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la
Ramadhani ambaye yuko mahututi katika wodi namba nane katika hospital ya
wilaya ya Geita.
Hata hivyo
watu wengine watano ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja
walitibiwa na kuruhusiwa kutokana na hali zao kuwa nzuri.
Jeshi la
polisi Wilayani Chato na Geita lilifika eneo la tukio hilo majira ya saa
4:30 na kukuta uharibifu mkubwa umekwishafanyika ikiwa ni pamoja na
kukuta duka la Mwenyekiti wa BAKWATA wilaya ya Chato Yusuph Idd
linalotumika kwa biashara ya M-Pesa na vinywaji baridi likiwa
linateketea kwa moto uliodaiwa kuwashwa na waumini wa dini ya kiislam.
Mkuu wa
Wilaya ya Chato Ludorick Mpogolo aliyefika eneo la tukio muda mfupi
baada ya polisi kuwasili eneo hilo mbali na kusikitishwa na kitendo
hicho aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati serikali ikiangalia njia sahihi za kutatua mgogoro huo ambao unakuwa kwa kasi kila kukicha.
Akizungumza
kwa njia ya simu na gazeti hili mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said
Magalula mbali na kuthibitisha kuwepo kwa tukio hilo, alionyesha kukerwa
na watu ambao wanafurahia vurugu zisizo na msingi na kuonya
kuwashughulikia wale wote watakaobainika ni wachochezi wa masuala ya
kidini.
KAMILI KWA HISANI YA http://1.bp.blogspot.com
No comments:
Post a Comment