Saturday, March 30, 2013

DALADALA NA BODABODA ZAGONGANA USO KWA USO

Kjina mmoja dereva wa boda boda yenye namba za usajili namba T  755 BYB amenusurika  kifo mara baada ya kupata ajali katika eneo la rombo /kibo  barabara ya morogoro  alipokuwa  akijaribu kukatiza kwa kasi mbele ya dala dala jana majira ya  moja na nusu usiku.

Ajali hiyo ilitokana na kijana huyo ambaye majina yake hayakufahamika haraka  alipokuwa akiingia bara bara kuu maarufua hapa jiji kama morogor road na kugongana uso kwa uso na dala dala  aina ya coster  linalofanya  safari zake kati ya Mbezi na Muhimbili.

Daladala hiyo ilikuwa ikitoka mjini kuelekea Mbezi ndipo ilipopata ajali hiyo na dereva  baada ya kuona  dereva wa boda boda amenguka chini na kutulia alitelekeza gari na kukimbia lakini  baada ya muda mfupi alikuwa chini ya madereva  bodaboda waliojitolea kumkimbiza na kumkamata na kumrudisha sehemu ya tukio  ,huku wakiwa  wamesha mpiga kwa kitendo chake cha kukimbia ,

baada ya tukio hilo nae kondakta wa dala dala hiyo alitokea katika kiza asijulikane wapi alipoelekea kitendo kilichowafanya abiria kushuka na kuanza kutafuta usafiri mwingine


mpaka naondoka sehemu ya tukio dervea wa boda boda laikuwa ameshapelekwa katika  hosipitali ya jirani huku dereva wa  daladala akiwa bado ameshikiwa na madereva bodaboda kusubiri askari wa usalama barabarani.

No comments:

Post a Comment