Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es
salaam jana akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea
mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu jana Machi 29,
2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili walikuwa wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa
mahututi. Juhudi zilikuwa bado zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye
kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa
ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova na Mkuu wa Mkoa huo Mhe
saidi Meck Sadiki katika eneo la jengo lililoporomoka mtaa wa Indira
Ghandi jijini Dar es salaam
Hadi kufikia leo asubuhi ni maiti nne tu ndizo zimedhibitishwa kuokolewa na jeshi la polisi na bado jeshi la wananch tanzania ,polisi na vikosi mbali mbali pamoja na mashirika mbali mbali pamoja na ya watu binafsi bado walikuwa wakiendelea kutoa misaada ya hali na mali ili kuhakikisha kuwa zoezi la uokoaji lina kamilika kwa muda muafaka.
wakati zoezi hilo likiwa linaendelea tayari jeshi la polisi limedhibitisha kumkata mmliki wa jengo hilo mara baada ya kujisalimisha m wenye mikononi mwa polisi pia jeshi la polisi limedhibitisha kuwatia mikoni maafisa watatu walikuwa wakifuatilia ujenzi wa jengo hilo
maafisa hao wanaoshikiliwa ni pamoja na mhandisi mkuu wa jengo hilo ,mhandisi wa manispaa pamoja na mkaguzi wa jengo hilo ili waweze kusaidi uchunguzi zaidi kuhusu kuanguka kwa jengo hilo lenye urefu wa ghorofa 15
No comments:
Post a Comment