leo asubuhi majira ya saa mbili na nusu macho na msikio ya watu waengi yalielekea katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu ambapo leo Sheikh Ponda Issa Pondaalifikishawa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam .
shekhe ponda na wenzake 49 wanatuhumiwa kwa kuvamia eneo la Markaz, Chang'ombe jijini Dar es Salaam, ambapo waliharibu na kuiba mali mbali mbali zenye thamani ya shilingi milioni 59.
hata hivyo Hakimu huyo alikubali watuhumiwa kuendelea na dhamana kwa washtakiwa wote isipokuwa kiongozi huyo ambaye ni mshtakiwa namba 1 kwa madai kuwa bado Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), hajaondoa pingamizi lake la kuzuia dhamana kwa mshtakiwa namba moja.
Ulinzi katika mahakama hiyo ulikuwa ni mkali na haujawahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni, ambapo pamoja na mambo mengine, palifungwa CCTV Cameras, vifaa vya kugundua vitu vyenye asili ya chuma, polisi wa kutuliza ghasia magereza na wale wa FFU, polisi wa farasi na mbwa, pamoja na askari kanzu waliotapakaa kila kona ya maeneo ya jirani na mahakama hiyo kubwa jijini Dar es Salaam.
Kikundi kidogo cha wafuasi wa Sheikh Ponda,walikuwa bado nje ya eneo la mahakama hiyo mara baada ya kuzuiliwa na askari polisi kuingi mahakamani hapo kwa madai kuwa wao ndio wanaosababisha vurugu mahakamani hapo .
hali ya shekhe Ponda ni ya kuridhisha na alikuwa na tabasamu la namna yake pale alipokuwa anaongea na mawakili pamoja na ndugu jamaa narafiki waliofiki mahakani hapo ,ambapo atafikishwa tena tarehe 2/05/2013 kwa kesi kutajwa na tarehe 09/05/2013 ndio siku ya kutoa hukumu dhidi yao.
No comments:
Post a Comment