Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi akihutubia baada ya zoezi la kuondoa kifusi kumalizika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Sera), William Lukuvi, akitoka eneo la tukio mara baada ya Dk. Nchimbi kuhutubia.
Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Nyambacha (kulia) akitoka eneo la tukio na makamanda wengine.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, DCP Suleiman Kova,
akitoka eneo la tukio, kushoto kwake ni mwandishi wa habari akimdodosa
jambo.
ILE operesheni ya kufukua kifusi cha ghorofa iliyoanguka jijini Dar
es Salaam imehitimishwa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi. Jumla ya maiti 34 zimepatikana na watu waliojeruhiwa
na kuokolewa wakiwa hai ni 18.
(PICHA: Haruni Sanchawa na Gladyness Mallya)
No comments:
Post a Comment