Monday, April 1, 2013

WATU 17 WAHOFIWA KUFA NA MIILI 13 YA WATU YAOPOLEWA MARA BAADA YA KUANGUKA KWA KIFUSI HUKO ARUSHA

                                      ENEO LA TUKIO 

                                        MMOJA WA M AJERUHI 

 MOJA YA MWILI WA MAREHEMU  ULIOTOLEWA KWENYE KIFUSI

 Wananchi wa eneo hilo wakiwa na simanzi baada ya ajali hiyo.
(Picha zote na www.wavuti.com)

habari  za kuaminika kutoka katika chanzo kimoja jijini Arusha wapakiaji  17 wanahofiwa kufariki dunia na tayari miili ya marehemu 13  imeshatolewa kutoka katika kifusi cha kokoto(moramu) huko Arusha.

akiongea na sambweti.blogspot.com kwa njia ya simu shuhuda wa tukio hilo kutoka Arusha anasema tukio hilo limetokea leo majira kati ya saa 4 na saa 5 asubuhi mara baada ya kuanguka kwa kifusi cha kokoto wakita wapaikiaji hao wakiwa shimoni wakipakia kokoto.

ajali hiyo ya kuanguka kwa kifusi imehusi magari mawili kufukiwa na kokoto ambapo ni lori  lilojulikana kama chombo cha neena pamoja na lori aina ya scania amabyo mpaka sasa bado yamefukiwa na kokoto pia yameharibika vibaya hivyo namba zako kushinda kutambulika mara moja.

 uokozi bado unaendelea ili kutoa miili ya wale waliokutwa na  tukio hili na pia jitihada zinafanyika kama kutaopolewa wengine wakiwa hai.

mlima wa moram uko nje kidogo ya jiji la Arusha katika eno la pekas kama unaelekea nduruma  mbele kidogo ya mji wa  Moshono

tayari mh mbunge wa ARUSHA GODBLESS LEMA na MH NASARI mbunge wa ARUMERU MASHARIKI wapo kwenye tukio la ajali kufuatilia hatua za uokoaji 

Mungu ametoa na Mungu  ametwaa jina lake lihimidiewa sambweti.blogspot.com linatoa pole sana kwa wahanga wa tukio hili.

No comments:

Post a Comment