Mwanamuziki mkongwe na bloggers, John Kitime wa pili kutoka kushoto, akiwa na vijana wake,Ahmad michuzi, kushoto kwake, King Kif, Sufiani Muhdin Sufiani na Salehe Ally ambao wote ni vijana wanaofanya vyema katika blog zao.
Akina dada hawa walikuwa wakishindana kucheza chakacha katika hoteli ya New Africa katika tukio hilo lililoandaliwa na Tigo Tanzania.
Cathbert Angelo akikabidhiwa IPAD yake baada ya kushinda katika shindano la kucheza muziki kwa wanaume.
Mkurugenzi na Mmiliki wa Bloger ya Kajunason Blog, Cathbert Angelo, Ijumaa ya jana ilikuwa na bahati kwake baada ya kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha kucheza muziki lililoanadaliwa na Kampuni ya Mtandao wa Simu za Mikononi ya Tigo Tanzania, katika siku maalum ya kufurahia na wamiliki wa blog mbalimbali katika Hoteli ya New Africa.
Party hiyo ilianza saa moja jioni na kumalizika saa nne za usiku, baada ya kumalizika kwa taratibu mbalimbali zilizoandaliwa na mtandao huo kwa ajili ya kuheshimu na kuthamini mchango wa magazeti tando, yani blog.
Mbali na Angelo, watu mbalimbali katika party hiyo walifanikiwa kujishindia simu, katika tukio hilo lililokutanisha bloggers wengi kwa wakati mmoja na kujadiliana mambo mbalimbali kwa ajili ya kuboresha kazi zao.
Hapa Salehe Ally, Muhdin Sufiani, Cathbert Angelo na Richard Mwaikenda wakijadiliana jambo katika Usiku wa Bloggers New Africa Hotel jana.
Watu weweeeeeee. Hapa jamaa wanaonyesha uwezo wao sasa. Kama unavyowaona. Kushoto ni Rajabu Mhamila Super De wakati kulia kwake ni Cathbert Angelo ambaye mwisho wa siku aliibuka kidedea. Duh, jamaa ni wakali vibayaaaaa.
picha na habari kwa hisani ya fununu habari blog.
No comments:
Post a Comment