Bw. William Mpinga, Tigo's Brand Manager kushoto na kulia ni Elias Bandeke mwakilishi wa Tigo |
Tigo Tanzania leo imenzindua huduma mpya ya malipo kwa kutumia simu ,huduma hii itamuwezesha mfanyabiashara kuuza bidhaa zake kwa mteja kuweza kununua bidhaa mbali mbali kwa kutumia laini ya tigo iliyoungnisha na huduma ya Tigo pesa.
Bw. William Mpinga, Tigo's Brand Manager kushoto akielezea kwa undani kuhusu bidhaa mpya ya tigo ya nunua na uza na tigo. |
Akiongea na waandishi wa habari meneja masoko wa bidhaa mpya za tigo Bw.William Mpinga amesema ''Tigo daima iko mbele kuwaletea wateja wao bidhaa na huduma nzuri ili kuongeza dhamani na kurahisiaha maisha ya watanzania wote.
Tigo imedhamiria kuboresha maisha ya mtanzania kwa kutanua mipaka yake katika Tigo pesa ,kwa kugundua njia rahisi za mawasiliano ikiwepo huduma ya Tigo pesa katika kuweka na kutoa pesa.
Bw. William Mpinga, Tigo's Brand Manager kushoto akielezea kwa undani kuhusu bidhaa mpya ya tigo ya nunua na uza na tigo. |
Tigo kwa kutambua mahitaji ya mtanzania imeleta huduma ya kukuwezesha kununua na kuuza bidhaa kwa kutumia tigo pesa ,huduma hii ni rahisi na salama na sasa hauhitaji tena kubeba pesa nyingi ili kwenda sokoni kununua bidhaa ,simu yako yenye laini ya Tigo inatosha kununua na kuuza bidhaa .
Ili kupata huduma hii unahitaji kubofya namba hizi kwenye simu yako yenye laini ya tigo na ilyounganishwa na tigo pesa *150*01# na kufuata maelekezo jinsi ya kununua na kuuza bidhaa kwa huduma hii ambapo sasa unaweza kununua vitu mbali mbali kama vifaa vya baiskeli ,kupata huduma kwa mama ntilie kununua sado kwa wauzaji wliosajiliwa na tigo na bidhaa mbali mbali pasipo kuwa na gharama kubwa.
Sasa kwa kutumia huduma hii unaweza kupata huduma mahali ulipo iwe nyumbani ofisini au mahali popote pale ulipo chakufanya ni kuwasiliana na wakala wa Tigo alieidhinishwa na kupewa uwezo wa kutoa huduma za kuuza na kununua bidhaa popote ulipo hapa nchini
Bw. William Mpinga, Tigo's Brand Manager kushoto akielezea kwa undani kuhusu bidhaa mpya ya tigo ya nunua na uza na tigo. |
kwa kuanzia kutoa huduma hii tigo imefundisha mawakala elfu hamsini(50,000 ) ambao leo wameanza rasmi kutoa huduma hii na unaweza kupata huduma hii mahali popote nchini Tanzania ,idadi inatarajiwa kuongeza na pia hii ni fursa nyingine ya ajira kwa Watanzania.
No comments:
Post a Comment