Monday, May 27, 2013

WILFRED RUGANYIZI RWAKATARE ARUDISHWA RUMANDE HADI TAREHE 10 MWEZI WA SITA MWAKA HUU

Mahakama ya hakimu mkzai kisutu jijini Dae es salaam ,leo imemrudisha rumande mkurugenzi  wa ulinzi na usalama wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema ,Bwana  Wilfred Ruganyizi  Rwakatare hadi  tarehe 10 mwezi wa sita  mwaka huu atakapofikishwa  tena mahakamani.

Akiahirisha kesi hiyo ,hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi wa kisutu  mh; Sundi Fimbo ,amesema mahakama imelazimika  kuahirisha kesi hiyo na kumrudisha rumande  bwana Rwakatare  ,kwa kuwa hakimu  anayesikiliza kesi hiyo yupo likizo.



Tarehe 8 mwezi mei mwaka huu mahakama kuu ya rufaa jijini Dar es salaam ilimfutia mashitaka bwana Wilfred Ruganyizi  Rwakatare  mashitaka ya kuhusika na  ugaidi  na kumbakiza na  kesi ya  kuhusika na utekaji,kesi ambayo  ilimsababisha  kupelekwa rumande  na leo kufikishwa mahakamani.

Awali mkurugenzi huyo wa ulinzi na usalama wa chadema alikuwa akishitakiwa kwa tuhuma za kuhusika na  ugaidi pamoja na tuhuma za kuhusika na  utekaji  kesi amabyo leo imemrudisha  tena  rumande hadi  tarehe 10 mwezi wa  6 mwaka 2013 atakapofikishwa tena mahakamani.

Baada ya  kesi  kuahirishwa Bwana Wilfred alichukuliwa chini ya ulinzi mkali uliombatana na msafara wa magari pamoja na ving'ora ,huku nyuma wakiwaacha wafuasi wa chadema pamoja na ndugu jamaa na marafiki  waliofiki  kusikiliza kesi hiyo wakiwa na simanzi

Hakika wengi bado wako gizani  wakihoji sababu za msingi  za kuahirishwa kwa kesi hiyo huku wengine wakihoji  ni kifungu kipi cha sheria kinachomrudishsha mtu rumande kwa sababu  hakimu  yupo likizo?

je  ni uhaba wa mahakimu

au

Nivisingizio  vya  kuchelewesha kesi.

No comments:

Post a Comment