Chama cha wananchi cuf katika jiji la dar es salaam ,leo wametangaza rasmi tarehe ya kufanyika kwa mkutano wa wazi na wananchi utakao fanyika jumapili tarehe mbili mwezi wa sita saa nne asubuhi katika uwanja wa chama cha wananchi zilizopo buruguni ambapo ni makao makuu na ngome ya chaho hapa jiji.
Mkutano huo wa siku ya jumapili mgeni rasmi anatarajiwa kuwa katibu mkuu wa chama cha wananchi cuf, Proffesa Ibrahim Lipumba ,
Katika mkutano wanataraji kujadili na kutoa elimu kuhusu gesi pia wanatarajia kufikia maadhimio kuhusu rasilimali gesi ambapo maadhimio yatakayopata mashiko , yatawasilishwa kwa mheshimiwa waziri mkuu na pia kwa mheshimiwa rais kwa utekelezaji wa haraka wa maadhimio hayo.
Mkutano huu utakao wahusisha wananchi watokao lindi na mtwara waishio dar es salaam ,utafanyika jumapili ,zikiwa ni siku kadhaa tu zimepita tangu kutokea kwa vurugu mkoani mtwara ,baada ya wananchi kupinga kusafirishwa kwa malighafi hiyo kutoka mtwara kuja Dar es salaam.
Ama kweli vita haina macho ni msemo wa katibu mkuu wa chama cha wananchi bwana Julias mtatiro ,alipokuwa anamalizia kutangaza rasmi kufanyika kwa mkutano huo siku ya jumapili tarehe 2 saa nne asubihi katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni sokoni jijini Dar es salaam.
Ewe mwananchi mpenda maendeleo ,fika katika mkutano huo siku ya jumapili kwa maendeleo ya nchi yetu.
picha zimepigwa na kasimu bruku wa jambo leo
|
No comments:
Post a Comment