Wednesday, May 29, 2013

SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA LATOA TAMKO JUU YA NGWEA NA M to The P


Shirikisho la Muziki Tanzania (Tanzania Music Federation) tunasikitika kutangaza kifo vya msanii  ALBERT MANGWEA kilichotokea Afrika ya Kusini akiwa kwenye shughuli zake za kimuziki .

Tunawapa pole Wazazi, ndugu, jamaa na watanzania wote kwa kuondokewa na mwanamuziki huyo mkongwe wa kizazi kipya, marehemu tutamkumbuka kwa mengi hasa msimamo aliounesha katika mambo aliyoyaamini, Alikuwa ni mtu mwenye jitihada hata mauti ilipomkuta alikua kwenye kujitafutia riziki.

 Marehemu alitambulika sana katika tasnia ya muziki kupitia wimbo wa GETO LANGU TU na baadae alirekodi nyimbo nyingi zilizopendwa na jamii ya watanzania.

Tunawaomba watanzania wazidi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu, Shirikisho lenu lipo imara na tunashiriki kikamilifu katika msiba huu tukishirikiana na wadau mbali mbali.


Tunapenda kuwatangazia kuwa Shughuli nzima ya mazishi ya mpendwa wetu ALBERT MANGWEA zitasimamiwa na Familia ya Marehemu, Shirikisho la Muziki kupitia chama cha Muziki wa kizazi kipya na wadau mbali mbali.

Kwa sasa tunakamilisha taratibu zote za awali, maandalizi na ratiba mzima itatoka baadae. Tulifanya kikao  na kaka wa marehemu (KENNETH MANGWEA) na kukubaliana kuwa msiba utakuwa MBEZI BEACH eneo la GOIG kwa sasa tunashirikiana vyema katika kukamilisha haya.

Kama mambo yatakwenda sawa, ikiwa ni pamoja na kuuleta mwili wa marehemu tunatarajia kuaga siku ya Jumamosi na baadae kusafirisha kwa shughuli ya Mazishi huko Morogoro eneo la Kihonda nyumbani kwa mama yake mzazi MAMA DENISIA MANGWEA.

Tunaomba tushirikiane sote kwa PAMOJA katika katika kipindi hiki kigumu. Taarifa zaidi tutawapatia baadae kadri itakavyo bidi.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana Lihimidiwe.Vile vile tunampa pole mwanamuziki Mgaza Pembe (M TO THE P) na kuomba maombi ya watanzania kumuombea mwanamuziki huyo  ambaye aliyekuwa Afrika Kusini na Marehemu. M TO THE P amelazwa Afrika Kusini.

Tunamuombea apone haraka.

Addo November Mwasongwe (Pichani juu)
Raisi Shirikisho la Muziki Tanzania
0713396367/0754396367
29th May 2013.

No comments:

Post a Comment