Sunday, May 5, 2013

HABARI UTOKA JIJINI ARUSHA KANISA KATOLIKI LA MT. JOSEPH MFANYAKAZI WA PAROKIA YA OLASITI ARUSHA lalipuliwa na bomu .


Habari kutoka Arusha zinasema watu wawili wamekamatwa kwa tuhuma za kuhusika na  mlipuko wa bomu lilitokea leo asubuhi katika kanisa   KATOLIKI LA MT. JOSEPH MFANYAKAZI WA PAROKIA YA OLASITI ARUSHA .

kanisa hilo leo ndio lilikuwa linazinduliwa  na balozi wa papa hapa nchini na watu kadhaa wameumia vibaya na kupelekwa katika hospitali ya mkoa ya Mt Meru kwa matibabu zaidi.


nikiongea na miliki wa blog ya haazu.blogspot.com taarifa kutoka polisi zinasema kuwa watu hao wawili wameshikiliwa na polisi na tayari hatua za upelelezi zimeanza ili kubaini kisa cha wao kwenda kulipua kanisa hilo.


aidha kamanda wa polisi amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mpaka sasa majeruhi wameshafikishwa hospitali na mpaka sasa hakuna taarifa kamili juu ya vifo kutona na tukio hilo la bomu lililotokea katika kanisa la katolika mt joseph mfanyakazi  la huko olasiti arusha.


mpaka muda huu mbunge wa Arusha mjini GODBLES LEMA ameshafika katika eneo la tukio kwa hiyo endelea kusoma blog hii kupata habari zaidi.


No comments:

Post a Comment