Jeshi la polisi kanda
maalum limefanikiwa kukamata majambazi watano ,Smg moja,Bastola mbili,magari
mawili ,matairi kumi,pikipiki moja pamoja na pingu.
Akiongea na waandishi wahabari
ofisini kwake kamanda wa kanda maalum DCP Suleiman Kova amesema jeshi la polisi
kanda maalum mnamo tarehe 22/05/2013 majira ya saa tano
asubuhi limefanikiwa kukamata majambazi 5 waliopora maeneo
ya Mbagala rangi tatu ,wilaya ya Temeke muda
mfupi baada ya kupora .
Tukio hilo lilitolewa taarifa
na mfanyabiashara amabye aliibiwa alipokuwa
dukani mwake katika duka la kuuza bia na ghafla alivamiwa na
majambazi watano watatu kati yao akiwa na silaha kubwa na
bastola mbili na kuporwa pesa taslim milioni arobain na sita (46,000,000.)
pesa ambazo alikuwa ameweka kwenye box tayari kuzipeleka kwenye benki ya Boa.
Majambazi hao walikuja kwa kutumia
piki piki mbili aina ya boxer zenye namba za usajili T.311 CGE rangi
nyekundu na walimtishia mfanyabiashara huyo bila
kufyetua risasi na kufanikiwa kuiba kiasi hicho cha pesa na baada ya polisi
kupata taarifa hizo waliwakamata maeneo ya Chamazi na majini yao :
1;Benard Yohana Mashamba
2;Steven Thadeo
3;Adam Isidory
4;John Masambo Benja
watuhumiwa wote mara baada kuhojiwa
na jeshi la polisi walimtaja mwenzao John Tesha aliyekimbia na pesa hizo
katika tukio lingine jeshi la polisi
kanda maalum Dar es salaam limefanikiwa kukamata bunduki aina ya Smg no
wa2608199 na magazine moja isyo na risasa huko maeneo ya Mbagala
kimbangulile na polisi inawashikilia Saidi Ally na
maneno Yahaya Mohamed wakituhumiwa kwa matukio ya unyang’anyi kwa kutumia
silaha hiyo wakitumi ausafiri wa gari lenye namba za usajili T 323 CFN
na T 289 BYL .
polisi inamshikilia Erick Innocent
Mbise kwa tuhuma za kukutwa na piki piki m
oja aina ya Fekon rangi nyeusi noT 155 CHX pamoja
na pingu na mt uhumiwa ametambuliwa na matukio mbali
mbali ya wizi wa piki piki.
HIZI PIKI PIKI ZILIZOKAMTWA KWA MAKOSA MBALI MBALI |
wakati huo huo mnano tarehe
18/05/2013 katika msako ilipatikana gari aina
ya toyota corala ambapo namba yake halali ni T
509 BZQ ambayo iliibiwa tarehe 16/02/2013 nyumbani
kwa Salome Edward Kange kwa
kutumia funguo bandia na polisi inawashikilia Ally Musa na Rebeka Mpumba kwa
tukio hilo.
PICHA JUU NI GARI LILOKAMATWA BAADA YA KUIBIWA NA HIZO NAMBA HAPO NI NAMBA ZA PIKI PIKI |
katika tukio la pili gari namba T 861
BGU toyota noah yenye namba za usajili T 897 BLV liloibiwa
tarehe 26/01/2013 nyumbani kwa Honory Kilipo Kobero huko Kimara
Temboni lilikamatwa tarehe 10/05/2013 huko Magomeni na
polisi inawashilikilia watuhumiwa wawili ambao ni Augustino
Kirunde Sanga na Jeremiah Nzashe Eliasi kwa kuhusika na tukio hilo.
Aidha jeshi la polisi kanda maalum
inawashikilia Elias Mohamed ,Nasiri Abdi na Deo John kwa
tuhuma za kukutwa wakipakia matairi kumi kwenye gari no T 346 BVB
matairi ambayo yaliibiwa katika godown.
kamanda Suleimani Kova amemamliza kwa
kusema jeshi la polisi limejizatiti kutoa ulinzi na usalama kwa raia
wote na kukanusha habari zilizozagaa kuwa walishindwa kutoa
ushirikiano katika tukio la wizi wa milioni arubain na sita kwa
kuonyesha silaha zilizokamatwa katika tukio hilo na kusema polisi
linawashikilia watumiwa wa tukio hilo huku wakifanya msako mkali kumkamata
jambazi aliekimbia na fedha hizo.
No comments:
Post a Comment