Wednesday, May 8, 2013

KESI YA FABIAN MASHAKA SAMBWETI Vs CHRISTINA MARIALE MADAI YA SHAMBA YAPIGWA TAREHE HADI 24-25 MWEZI WA SABA MWAKA HUU

Habari kutoka jijini Arusha zinasema kuwa kesi  ya madai ya kudhulumiwa shamba  dhidi ya  familia bwana Fabiana  Mashaka sambweti ambaye ni  mmililiki halali wa shamba na mlalamikiaji  Andrew  Mollel  imehairisha na mahakama ya ardhi leo Asubuhi  hadi tarehe 24-25 mwezi 7 2013  itakapo sikilizwa tena.

kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka 2006  na mama mzazi wa ANDREW MOLLEL kwa madai kuwa bwana Fabian Sambweti   amevmia shamba hilo lenye ukubwa wa zaidi ya ekari mbili lilipo mkabala na  magorofa ya AICC kijenge  mjini arusha  kudai kuwaa  hali hiyo  imemsababishia  mmiliki ambaye ni Andrew Mollel  kushindwa kufanya shughuli zake za kimaendeleo .

Mhe hakimu Mungure   leo ameipiga tena tarehe kesi hiyo ikiwa ni muda mrefu wa zaidi ya miaka 6  ikiwa inapigwa dana dana  kwa madai kuwa mlalamikiji anadharura ana leo hii mlalamikaji amefika  mahakamani hapo na kudai kuwa vielelezo vyake vyote vya umiliki wa shamba  hilo vimepotea hivyo amekuja na  taarifa ya upotevu  inayotolewa na  polisi ili k udhibitisha  madai yake.



kesi hiyo ni mara ya pili ikifika mahakamani ambapo mmiliki wa shamba hilo Bwana Fabian Masahaka Sambweti alishafikishwa tena kwa pilato kwa kesi hiyo hiyo  kujna kipindi alifikishwa kwa mhe ELIATONGA MREMA  na mwisho wa siku mwaka  1994 bwana Fabiana alishinda kesi hiyo na kukabidhiwa shamba hilo .

Mwaka  2007 mwanae mmoja jina kapuni  alianza ujenzi wa nyumba  ya kuishi katika eneo hilo  nyumba yenye  ukuwa wa vyumba vitatu,jiko,sebule na chumba kulia  chakula pamoja na  malito  lakini alipofikisha tu sehemu ya kupauwa bati alipata barua kutoka mahakama ya Ardhi ya kusismsmisha ujenzi huo mara  moja.

Familia ya bwna  Fabiani Sambweti na kijana wao huyo walitii sheria ya mahakama  ambapo mpaka leo bado wanasubiria  kujua nini hatma ya kesi hiyo na nini hatma ya ujenzi wa hiyo nyumba  uliosimama kwa takrbani miaka  7 sasa huku baadhi ya vifaa   kama , sement, mbao na  vifaa vingine vikiwa tayari vimeshaharibiki kwa kukaa muda mrefu.

kwa muendelezo na kujua nini kimeendelea huko mahakamani fuatili   tarehe 24/25 ambapo keshi hii itasikilizwa tena katika mahakama ya Ardhi jijini Arusha.

kwa  habari  zaidi kuhusu kesi hii endelea kufuatilia http://sambweti.blogspot.com


No comments:

Post a Comment