Saturday, May 25, 2013

PIKI PIKI 300 ZAKAMATWA NA POLISI WAKATI HUO HUO POLISI WAJIANDAA NA UJIO WA RAIS WA MAREKANI MH :BARACK OBAMA

Jeshi la polisi kanda maalum Bar es alaam ,katika kuhakikisha usalama wakati wa ujio mkubwa wa  rais wa Marekani mh  barack obama siku chache zijazo ,jeshi limehimarisha usalama  katika jiji zima la  Dar es salaam  likishirikiana na vyombo vingine vya usalama , ili kuhakikisha  wageni wote wanakua salama  wakati  wa ujio wa rais Barack Obama.

Akiongea na waandishi wa habari kamanda wa kanda maalum suleiman kova amesema wanajiandaa vizuri  kuhakikisha usalama kwa wageni wote wanaoingia na kutoka katika jiji la Dar es salaam kuhakikisha wanaingia na kutoka salama .

Akielezea ujio huo k amanda amesema wanategemea ujio mkubwa  katika jiji la Dar es salaam na kuomba wananchi kuwapokea wageni hao na kuwasidia pale wanapohitaji msaada ,na  kuwakumbusha wananchi  kutoa  taarifa zozote  za  kutishia usalama kwa raia, pamoja na  wageni hao, kwa kutoa   taarifa haraka kwa vyombo vya sheria ili hatua zaidi   ziweze  kuchukuliwa dhidi yao.

Aidha jeshi la polisi kanda maalum Dar es salaam limekamata piki piki    300 kati ya hizo piki piki 201 ni aina ya Boxer, piki ambazo zimekuwa tishio katika jiji la dar es salaam kwa tuhuma za kutumika katika uhalifu, amesema jeshi linashikilia piki piki hizo kwa uchunguzi zaidi kubain uhalali wa piki piki hizo mara baada ya jeshi hilo kubain kuwa zinatumika zaidi katika uhalifu.


Kamanda amewadhibitishia  wananchi wa jiji la Dar es salaam kuwa wamejiimarisha vilivyo kupamambana na  vitendo vyote dhidi ya uhalifu  na kusema hakuna  mtu yeyote yule au jambazi atakayeweza kufanya vurugu au kufanya uhalifu   bila kuchukuliwa hatua za kisheria.

No comments:

Post a Comment