MENEJA MASOKO WA TIGO NA MENEJA WA FASTJET BWANA TIM LEE-FOSTER |
PICHA YA PAMOJA TIGO NA FASTJET |
WAANDISHI WA HABARI MBALI MABLI WAKIFUATILIA MAELEZO YA MENEJA MASOKO WA TIGO BWANA WILLIM MPINGA |
Akiongea na waandishi wa habari jana katika hotel ya Atlantis ya jijin Dar es alaam Meneja mauzo wa Tigo bwana William Mpinga amesema wamezindua rasmi huduma ya kununua tiket za kusafiria za ndege za shirika la fastjet mara baada ya shirika hilo kuona mafaniko ya huduma ya tigo pesa na huduma ya Nunua na uza chochote na Tigo pesa kuzinduliwa hivi majuzi.
Muungano huo wa kirafiki wa biashara baina ya Tigo na Fastet unalengo la kumrahisishia Mtanzania katika kupata huduma za fast jet na kuokoa muda wa kwenda ofisini kuandaa tiket ya safari , a kusema huduma hiyo sasa inapatikna mikononi mwako kwa kutumia simu yako yenye lain ya tigo ambayo imeunganishwa na huduma ya Tigo Pesa.
Ili kupata huduma ya kununa tiket ya Fastjet ni rahisi sana kwako mtumiaji wa Tigo piga *150*01 na ufuate maelekezo ambayo yatakupeleka mpaka uweze kununua tiket yako ya fast jet popote pale ulipo nchini Tanzania
Nae akionge baada ya uzinduzi huo wa nunua tiket ya fast jet na tigo pesa meneja wa fast jet bwana TIM LEE-FOSTER amesema bado wataendelea kuleta huduma mpya zaidi na nzuri kutoka Fastjet na kusema ,pamoja na mafaniko makubwa waliopata baada ya kuwa na huduma ya nunua tiket na fastjetbado wanamalengo makubwa ya kupanua biashara ya Fastjet kwa kuwa karibu na jamii nzima ndio sababu wakakubali kuungana na Tigo kwani tigo ipo mstari wa mbele kutoa huduma kwa jamii ya Tanzania wakati wote.
Akimalizia kuzindua muungan huo wa kibiashara baina ya fastjet na Tigo Tanzania, Mpinga amesema hii ni hatua kubwa kufikiwa baina Tigo na Fastjet na kuwaahidi watumiaji wa Huduma za tigo huduma bora kwa wateja wake waote waliojiunga na huduma ya TIGO PESA.
UNANGOJA NINI JIUNGE NA TIGO PESA UPATE HUDUMA BORA KUTOKA TIGO PESA
No comments:
Post a Comment