Wednesday, June 19, 2013

Chama cha Wananchi (CUF) chalikosoa Jeshi la Wananchi (JWTZ)

Naibu mkurugenzi wa Habari Uenezi na Haki za Bindamu, Abdual Kambaya

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UNYAMA UNOFANYAWA NA JESHI LA WANANCHI-MTWARA
TEREHE: 19/06/2013
Baada ya vurugu zilizoendelea Mtwara jeshi la Wananchi (JWTZ) lililopewa dhamana ya kulinda amani ya mji ya Mtwara limekuwa  likikiuka haki za watanzania hao wa Mtwara kwa kuwafanyia ukatili usiofaa watanzania hao, bila hatia yoyote.
CUF Chama cha Wananchi kimeshuhudia wanajeshi hao walioko Mtwara wakipiga raia bila hatia,kuwateka na kuwapeleka kwenye kambi ya jeshi na kuendeleza mateso yasiyo na hatia.Miongoni mwa mateso wanayopewa raia hao ni  kurushwa kichura bila kujali ni wazee,wanawake,wajawazito ama wagonjwa.
Hivi sasa wanajeshi hao wamekuwa wakiendelea na harakati za kuwakamata viongozi wa chama cha wananchi CUF na kuwapeleka kambini na kuwapa adhabu mbaya.Hivi karibuni wamemkamata Mkurugenzi wa Siasa wa CUF mkoa wa Mtwara  Bw.Saibogi.Naye mkurugenzi wa Haki za Binadamu wa CUF imebidi akimbilie porini huku wanajeshi hao wakimsaka kwa udi na uvumba.
Katika hali isiyo ya kawaida wakati wa uchaguzi wa madiwani uliofanyika Jumapili iliyopita walipeleka vifaru kwenye maeneo ya uchaguzi na wanajeshi zaidi ya ya 400.Hali hii imepelekea hofu kwa wapiga kura na  zaidi ya wapigakura 3000 hawakujitokeza kwenda kupiga kura wakihofia usalama wao inayotokana na vitisho vya wanajeshi hao.
Wanajeshi hao hawakuishi hapo tu bali wamediriki kutishia hata mawakala wetu wa kusimamia uchaguzi hali ambao imepelekea kuinyang’anya CUF uishindi na kuipa CCM.
CUF chama cha Wananchi hakikubaliani na hali hii ovu  nay a kihalifu inayofanywa na Serikali ya CCM kupitia JWTZ ambalo sasa linatumiwa kisiasa.Hivi sasa tunalitafakari kwa uzito jambo hili na muda mfupi tutatangaza hatua tutakayochukua.
Imetolewa na
Abdual Kambaya
Naibu mkurugenzi wa Habari Uenezi na Haki za Bindamu

0719566567

No comments:

Post a Comment