Wednesday, June 19, 2013

Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma barani Afrika nchini Ghana


Watanzania wakipunga mikono wakati wa ufunguzi wa mikutano ya watumishi wa umma barani Afrika unaofanyika chini Ghana.
Ofisa Tawala Mwandamizi wa Wizara ya Fedha, Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Merkion Ndofi (kushoto), akimkaribisha mwananchi wa Ghana katika  banda la Wizara ya Fedha.
Ofisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi wa Wizara ya Fedha, William Ghump (kulia), Mkurungezi wa Utawala na Utumishi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Peter Mapigano (kushoto) na Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, wakipanga mkakati wa uelimishaji umma katika banda la Wizara ya fedha katika maonesho ya maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma, barani Afrika nchini Ghana leo. 
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha, Christina Ngonyani akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa Ghana kuhusu umuhimu wa mikopo kwa Watumishi wa  Serikalini, wakati wa mkutano huo.
Ofisa Tawala Mwandamizi wa Wizara ya Fedha, Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Merkion  Ndofi akiwaeleza wanafunzi wa Ghana juu ya utendaji kazi wa Idara ya Utawala katika wizara ya Fedha, nchini Ghana leo.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo ya Watumishi wa Umma wa Wizara ya Fedha, Christina Ngonyani akiwa na Ofisa Tawala Mwandamizi, Merkion Ndofi, wakitoa ufafanuzi  kuhusu utendaji wa kazi za Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali  kwa wageni waliotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonesho ya Wiki ya Utumishi barani Afrika nchini Ghana.
Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi, Peter Mapigano (kulia) wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), akitoa maelezo juu ya utendaji kazi na huduma mbalimbali ambazo Benki ya Posta inatoa kwa wananchi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma, Celina Kombani (kulia), akiwa na Katibu Mkuu wake, George Yambesi, wakitembelea banda la Wizara ya Fedha nchini Ghana.
Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma akifafanua  jambo kwa Eugene Koranteng Henaku wa Umoja wa Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa nchini Ghana,wakati alipotembelea banda la wizara hiyo kwenye maadhimisho hayoleo. (Picha zote na Scola Malinga- Hazina -Tanzania)

No comments:

Post a Comment