JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
|
|
|
TAARIFA KWA UMMA
SERIKALI HAIJAFUTA MITITIHANI
YA TAIFA YA MASOMO YA DINI
Serikali inapenda kuwafahamisha wananchi kuwa
haijafuta Mitihani ya Taifa ya masomo ya Dini kama ilivyoripotiwa na baadhi ya
vyombo vya Habari. Masomo hayo ni pamoja
na Elimu ya Dini ya Kiislam, Bible Knowledge, Islamic Knowledge na Divinity.
Masomo ya Dini yanaendelea kufundishwa shuleni na
kutahiniwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
Hata hivyo, Serikali inakusanya maoni kuhusu namna
bora zaidi ya uendeshaji wa Mitihani ya Dini.
Imetolewa na:
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA
UFUNDI
01/06/2013
No comments:
Post a Comment