. Hii inaonyesha nakisi kubwa iliyoko ya upatikanaji damu kwenye hospitali
26%). Hii inaonyesha nakisi kubwa iliyoko ya upatikanaji damu kwenye
hospitali zetu. Nakisi hii mara nyingi imekuwa inafidiwa na ndugu kuchangia
damu ili kuokoa maisha ya mgonjwa. Lengo la Mpango ni kukusanya damu kwa
100% toka kwa wachangiaji damu wa hiari.Mikakati kadhaa imewekwa
kukabiliana na changamoto hii kama tutakavyoona baadaye.
Changamoto nyingine ni kama ifuatavyo;
- Uelewa mdogo katika jamii kuhusu suala zima la uchangiaji damu kwa
hiari kwani mfumo uliozoeleka ni ndugu wa mgonjwa kuchangia damu
- Uhamasishaji usiotosheleza toka kwa viongozi mbalimbali wa
jamii,wanasiasa,viongozi wa dini nk.
- Uuzwaji wa damu usio halali hospitalini jambo mbalo linawakatisha
tamaa wachangia damu wa hiari
- Matumizi yasiyo sahihi ya damu katika hospitali na
- Miudombinu hafifu hususan barabara duni wakati wa kukusanya na
kusambaza damu
Ndugu Wananchi
Mpango wa Taifa wa Damu Salama umeweka mikakati ili kukabiliana na
changamoto na kufikia malengo kama ifuatavyo;
- Kufanya kampeni ya kuhamasisha uchangiaji damu katika jamii
(Community Campaign), Kampeni hii ina lengo la kuhakikisha upatikanaji wa
damu ya kutosha wakati wanafunzi ambao ndio wadau wakubwa wapo likizo
- Kuongeza vituo vidogo vya kuchangia damu- “Blood collection satellite
sites” katika sehemu mbalimbali za nchi. Kwa sasa Mpango una vituo vidogo
vinne Dar-es-salaam- Mnazi Mmoja , Dodoma, Lindi na Morogoro ambavyo vina
uwezo wa kukusanya chupa za damu 18,000 kwa mwaka
- Kushirikiana na uongozi wa mkoa kupitia mganga mkuu wa mkoa ili wilaya
zitenge bajeti ya kukusanya damu kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa
damu salamaKufanya mkakati wa kujua matumizi halisi ya damu (Blood need
assessment) nchini na kuendelea kuhamasisha madaktari, wauguzi na
watumishi wa maabara juu ya matumizi sahihi ya damu
- Kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali Puplic Private
Partnership(PPP)
kuhakikisha Mpango unafikia malengo ya kukusanya chupa za kutosha za damu
- Kuendelea kuelimisha jamii kuhusu damu haiuzwi kwa kutumia vyombo vya
habari na vipeperushi pia kutumia vifungashio vya damu (Blood bag) vyenye
ujumbe “DAMU HAIUZWI”
- Kuendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii (nje ya shule na vyuo)
umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari
- Kutoa majibu, na ushauri nasaha ndani yawiki mbili mpaka nne baada ya
mtu kuchangia damu lengo ni kufikia 75% ya wachangiaji damu wa hiari
ifikapo mwishoni mwa 2014. Kwa sasa Mpango umeweza kutoa majibu na
ushauri nasaha kwa 58% ya wachangiaji damu wa hiari.
- Kuanzisha utaratibu wa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia ya
simu kwa wachangia damu. Ujumbe huo utakuwa wa kuhamasisha, kumkumbusha
mchangiaji siku ya kuchangia tena damu n.k
- Kuongeza utengenezaji wa mazao mbalimbali ya damu (Blood Products) toka
30% ya sasa mpaka 50% mwaka 2014.
- Kuongeza kiwango cha asilimia ya wachangia damu wa mara kwa mara kutoka
20% kwa sasa (Repeat donors), hadi 50%ifikapo mwaka 2015 . Mpango
utahakikisha unatembelea taasisi kwa ajili ya kuchangia damu angalau
mara mbili kwa mwaka.
Ndugu Wananchi;
Uchangiaji damu wa hiari wa bila malipo yoyote na wa mara kwa mara ni
msingi wa upatikanaji wa damu salama na ya kutosha. Wachangiaji damu wa
kujirudia ni salama kwani damu yao hainakiwango kikubwa cha maambukizo ya
magonjwa yanayoweza kuenezwa kwa njia ya damu. Lengo la Shirika la Afya
Duniani (WHO) ni kwa nchi zote kupata mahitaji yao yote ya damu
inayohitajika kutoka kwa wachangiaji wa hiari wasiolipwa ifikapo mwaka 2020
Ndugu Wananchi;
Natoa rai/ujumbe kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kuchangia damu kwa
hiari mara kwa mara ili nchi iwe na akiba ya damu ya kutosha , kwani
asilimia moja ya Watanzania wakiamua kuwa wachangiaji damu wa kujirudiaMpango
wa Taifa wa Damu Salama utaweza kukidhi mahitaji ya damu nchini.
NAMALIZIA KWA KUSEMA NAOMBA WANANCHI WAJITOKEZE KWA WINGI SIKU HIYO ILI
TUONYESHE MSHIKAMANO NA KUTOA ZAWADI YA MAISHA KWA KUCHANGIA DAMU. PAMOJA
INAWEZEKANA
No comments:
Post a Comment