Friday, February 28, 2014

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILWA MKOANI LINDI ATOA UFAFANUZI JUU YA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA JAMII KWA KUTUMIA FURSA YA GESI ASILIA

 MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA KILWA MH ADOH  AKIFAFANUA JAMBO WAKATI WA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM KULIA NI MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA KILWA MH ALLY MTOPA

 MH MKURUGENZI HALMASHAURI YA KILWA  BW ADOH MAPUNDA
 MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA KILWA MH ADOH  AKIFAFANUA JAMBO WAKATI WA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM
 MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA KILWA MH ADOH  AKIFAFANUA JAMBO WAKATI WA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM NA KULIA NI MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA KILWA MH ALLY MTOPA


 ENGINEER WA HALMASHAURI YA KILWA BWANA WAHABU YAHAYA  AKISIMAMA BAADA YA KUTAMBULISHWA KWA WAANDISHI
 KAIMU MWANASHERIA WA HALMASHAURI YA KLILWA  BWANA GODFREY  JAFFARY AKITAMBULISHWA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI
BWANA HASSAN ALLY  KATIBU  KAMATI YA WILAYA  YA KILWA


  BWANA LUKAS ELIAS NDOMBOLE  KATIKATI MWEKA HAZINA WA HALMASHAURI YA KILWA


 MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA KILWA MH ADOH  AKIFAFANUA JAMBO WAKATI WA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi Mh MAPUNDA ADOH  STEPHEN leo amaetoa ufafanuzi na hatua mbali mbali zinazochukuliwana na zinazotarajiwa kuchukuliwa na halmashauri ya  Wilaya hiyo ya kilwa ili kuboresha  huduma za jamii ya  halmashauri  ya Wilaya ya Kilwa walipokutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mh.ADOH huku akiwa ameambatana na mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya kilwa ya mkoani lindi Mh ALLY MTOPA ameweza kufafanua vyema  jinsi halmashauri yake ilivyojipanga katika kuhakikisha kuwa jamii ya wilaya ya Lindi inapata huduma zote katika wilaya yake,akiwa na mwenyekiti wa halmashauri  ya wilaya ya Lindi ,mkurugenzi  pia aliambatana na jopo zima la viongozi mbali mbali kutokyema na kupata katika Wilaya ya Lindi ambao wapi jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuhudhuria semina elekezi.
Katika kuhakikisha  huduma bora kwa jamii ya watu wa Halmashauri ya kilwa ,Mkurugenzi na jopo lake  wamesimama kuhakikisha kuwa rasilimali za ndani zinasimamiwa vyema ili kuhakikisha mapato yanafika katika sehemu husika ,mfano ushuru wa zaa ufuta,ushuru wa mauzo ya viwanja,ushuru wa gesi asilia ambapo asilimia 20% ya mapato hayo yanapelekwa katika kijiji cha songo songo

Miradi mingine na misaada inayotekelezwa na Songosongo
MRADI WA MAJI 
                                         Wananchi wa kijiji cha songo songo wanapata huduma ya maji safi  na salama toka kampuni ya PANAFRICAN AGENCY wastani wa lita elfu 30 kwa siku.

MRADI WA UMEME
Wananchi wa kijiji cha Songo songo wanapata huduma ya umeme bure ilimradi agharamie uingizaji

ELIMU YA CHEKECHEKEA
Wananchi wa Song  songo wamejengewa darasa  la chekechea  na kujiendeleza

ELIMU YA MSINGI
Wananchi wa Songosongo  wamepewa fursa ya kusomesha watoto 10 kila mwaka katika shule ya Makongo ya jijini Dar es Salaam

SHULE YA SECONDARY
Wananchi wa Songosongo  wamejengewa bweni la kulala watoto wa kike  lenye thamani ya 194,000,000.00/=
HUDUMA YA AFYA
Zahananati ya  Songosongo inapata  huduma ya madaktari toka PTA kwa wiki mara mbili
AJIRA
Miradi inayotekelezwa na wananchi  wa Songosongo  wanapewa  kipaumbele katika kupewa ajira
ULINZI NA USALAMA
Kwa sasa  serikali ina mpango wa kujenga kituo cha polisi cha kisasa chenye thamani ya Tsh.625,000,OOO.00/= na mchoro wake umekamilika huo hapo chini

VIPAUMBELE  VYA FEDHA ZA GESI
Baraza la madiwani katika vikao vyake mbali mbali vimepitisha na kutoa azimio kwa asilimia 36% yatokayo na  mapato ya gesi yatumike  katika sekta ya elimu kiasi kinachobaki  kinatumika katika kuboresha huduma zingine kama vile barabara ,afya na utawala
UJENZI WA BANDARI YA KILWA KIVINJE
Halmashauri imeanza kulipa fidia jingo moja linalomilikiwa na mtu binafsi  kwa lengo la kulikarabati  ili liweze kutoa huduma kwa jamii ,aidha halmashauri imeanza  mchakato w kutafuta fedha  za kujenga  ukuta wa kukinga mmomonyoko toka bandari na sio kujenga bandari.

MRADI WA KUKARABATI KITUO CHA AFYA KILWA –MASOKO
Mradi huu uko mbioni kuanza hivi karibuni

MIRADI MIKUBWA INAYOSHIRIKISHA WADAU  WA MAENDELEO

HOSPITALI YA KISASA
Kwa kushirikiana na wadau wa gesi ,wilaya ya kilwa inatarajia kujenga hospitali yenye hadhi  ya kimataifa ,tayari eneo  la ekari 30 limetengwa  na mchoro umekamilika huo hapo chini

UKUMBI WA MIKUTANO WA KISASA
Halmashauri  pia inatarajia  kujenga ukumbi wa mikutano wa kimataifa utakao gharimu takribani Tsh.3.8  billioni.kazi itafanywa kwa kushirikiana na UTT







AFISA MIPANGO YA HALMASHAURI YA  WILAYA YA KILWA  BWANA DANIEL T LUSINGU 







PICHA YA PAMOJA YA VIONGOZI MBALI MBALI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILWA  MKOANI LINDI 


KWA TAARIFA YAKO
KILWA imetangazwa na UNESCO kuwa sehemu muhimu yenye urithi wa duni a ,kuna vivutio  ya mambo ya kale ,ni eneo la utalii ,ustarabu na,samaki kwa wingi  sana.

No comments:

Post a Comment