Sunday, March 2, 2014

Kampeni za Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Kalenga

*Wananchi wafurika Kata ya Nzihi


Mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Mgimwa (32), akilakiwa kwa shangwe na vigeregere alipowasili katika Kijiji cha Magubike, Kata ya Nzihi, Iringa Vijijini, kufanya mkutano wa kampeni jana mchana.
Wafuasi wa CCM wakishangilia kwa nguvu wakati Mgimwa akihutubia kuwaomba kura. Uchaguzi wa Jimbo hilo la Kalenga utafanyika Machi 16, mwaka huu.
Mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa akiwa amebebwa na wafuasi wa chama hicho, alipowasili katika mkutano wa kameni katika Kijiji cha Ilalasimba, Kata ya Nzihi, Jimbo la Kalenga jana asubuhi.
Ni nderemo na vifijo kila mahali katika mkutano wa kampeni za CCM katika Kijiji cha Ilalasimba.
Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia chama hicho, Godfrey Mgimwa katika Kijiji cha Ilalasimba .jana
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba akihutubia mkutano wa hadhara kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, Gofrey Mgimwa katika Kijiji cha Magubike . (Picha zote kwa hisani ya Richard Mwaikenda wa Kamanda wa Matukio Blog)

No comments:

Post a Comment