*Atoa mazito ya moyoni.
*Ahidi kukimaliza chama hicho katika uchaguzi Jimbo la Kalenga
Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kata ya
Nzihi akijitambulisha rasmi kwa wananchi wa Kijiji cha Nzihi kuwa yeye ameamua
kuachana na chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa
hiari yake, baada ya kupima uwezo wa chama hicho na CCM katika Hoja na
Matendo.
Mwanachama
huyu mpya wa CCM, ameahidi kuongoza timu ya ushindi ya chama hicho,
kwenye Kata ya Nzihi kuhakikisha mgombea wake, Godfrey Mgimwa anapita
kuwa Mbunge.
Pia
amesema kuwa ataiweka wazi mipango ya chama chake cha zamani (Chadema)
na watu wageni wa Chadema waliokodishwa na kupangishiwa nyumba katika
Kata ya Nzihi, wanaotembea usiku kwa ajili ya kutafuta kura na
kushambulia waowaunga mkono CCM kwenye Kata ya Nzihi.
No comments:
Post a Comment