wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya Kajumulo Girls High School wakati wa kusherekea mahafali ya tatu
Wanafunzi wa Kajumulo Girls High School wanaohitimu kidato cha 6 wakati wa kusherekea mahafali ya tatu katika shule yao.
Kwa
niaba ya Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea na Mwana hisa wa “VIP
Engineering and Marketing Ltd” Mzee James Rugemalira aliyependa kuwa
nasi leo lakini akashindwa kutokana na majukumu mengine, tunayo furaha
kuwatangazia, kuwa VIP ataanzisha mfuko maalum wa kusaidia katika
kuboresha utoaji Elimu katika nchi yetu, utakaoitwa “Auleria Kobulungo
Muganda Memorial Education Foundation Trust”. Mfuko huu unaanzishwa kwa
heshima na kumbukumbu ya mzazi wetu mpendwa marehemu Ma Auleria
Kobulungo Muganda.
Mheshimiwa
mgeni rasmi, Tunayo furaha kutangaza kwamba shule yetu ya Kajumulo
Girls High school ndio itakuwa shule ya kwanza kufaidika na mfuko huu,
na leo, VIP kwa niaba ya “Auleria Kobulungo Muganda Memorial Education
Foundation Trust” imetoa jumla ya TZS 200 million (TZS 200,000,000) kwa
ajili ya kuwasadia baadhi ya watoto wasio na uwezo wa kujilipia lakini
wana sifa za kujiunga na kusoma katika shule hii.Baba Methodius Askofu Kilaini nae alitoa neno
Mkuu
wa Shule ya Kajumulo Girls High School Jospina Leonidace(kushoto) na
kulia ni Fr. Vitus Mrosso (Nyuma) katikati ni Mr. Adrew Kagya akiwa na
Rahim Kabyemela
Prof.
Anna Tibaijuka akiwa na Mgeni rasmi Mheshimiwa mgeni rasmi, Bi. Edwina
Lupembe, Mkurugenzi wa “Mkombozi Commercial Bank" kwa furaha
wakisikiliza Risala kutoka Wanafunzi wahitimu wa kidato cha sita
Taswira,
Wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita wakisoma Risala mbele ya Mgeni
rasmi Mkurugenzi wa Mkombozi Commercial Bank, Mama Edwina Lupembe na
viongozi mbalimbali Meza kuu.
Prof. Anna Tibaijuka (kulia) akiteta na Mwl. wa Shule hiyo ya Kajumulo Girls High School
Ni
matarajio yetu kuwa mchango huu utawafikia walengwa, wale watoto wenye
uwezo na nia ya kusoma, lakini wanatatizwa na karo pamoja na michango
mingine ya shule.
Tutashirikiana
na Uongozi wa Shule na Wataalam wengine kuweka taratibu za uwazi
zitakazoongoza uteuzi wa watoto watakao faidika na msaada wetu.
Ninaisihi sana kamati itakayohusika na uchambuzi wa watoto wanaofaa kwa
msaada huu itende kazi yake kwa uadilifu ili wale watakaochaguliwa
kuhudumiwa wawe wale wanaostahili huduma hii.
Pia,
ni matarajio yetu kuwa mchango wetu utakuwa kichocheo kwa watu wengine
kujitoa kwa hali na mali kusaidia shule yetu hii ili iweze kupiga hatua
zaidi katika jitihada za kutoa elimu bora kwa mtoto wa kike. Siku hizi
watu wengi wanaweka jitihada kubwa kuzungumzia matatizo, wakati wanaweka
jitihada kidogo katika juhudi za kuyatatua. Tukishirikiana kwa dhati
bila shaka tunaweza kupunguza matatizo ya watoto wetu.
Kwa
wale wanafunzi watakaohudumiwa na michango kama hii, ni mategemeo yetu
kuwa mchango huu utawaongezea bidii ya kusoma kwa kujiamini bila mashaka
kwamba watafukuzwa shule kwa kukosa karo au mahitaji mengine ya shule.
Tafadhali weka juhudi ili muweze kusoma vizuri, na mukimaliza shule
tuweze kuona matunda ya upendo wetu kwenu. Hakuna tunachodai kwenu, ila
mafanikio yenu katika maisha.
Wazazi nao hawakuwa mbali...Wazazi na walezi wa Wanafunzi Kwa Makini Wazazi wakiwaangalia watoto wao huku burudani ya ngoma ikiendelea..Ngoma kutoka Kidato cha kwanza.Watoto
wa Kidato cha kwanza wakicheza ngoma huku wakituzwa na Dada zao
wanahitimu masomo yao katika shule hiyo ya Kajumulo Girls High School ya
Wasichana.Wanafunzi wanaohitimu kidato cha Sita wakiwapongeza wadogo zao kwa kucheza vyema ngoma Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mkombozi Commercial Bank, Mama Edwina Lupembe akitoa neno.Mr. Andrew Kagya akitoa neno.
Kwanza
kabisa ni kudhihirisha kwamba VIP inagawana ndoto (VIP shares the same
Vision) na mwanzilishi wa shule hii Prof. Anna Tibaijuka, ya kumkomboa
mtoto wa kike ili aweze kujitegemea yeye mwenyewe, wale anaowategemea na
hatimae kukomboa Taifa zima. Ni imani yetu (Conviction) kwamba njia
bora ya kumkomboa mtoto wa kike ni kumpa elimu bora.
Ni
njia ya kuwapa fursa watoto ambao hawana uwezo wa kifedha lakini wana
sifa zinazotakiwa kupata elimu bora. Ni wakati wa kuwaonesha watoto hawa
kwamba pamoja na ubinafsi unaongezeka katika jamii, bado kuna watu
wanaowajali na kuwathamini. Watu ambao wako tayari kuona hata wao
wanapata fursa ya kufanikiwa katika maisha. Watoto hawa wakitambua
vizuri thamani ya mchango huu, wakatambua thamani ya upendo wa Taifa
kwao, na hiyo itawajengea moyo wa kuwasaidia wale ambao hawana uwezo
wakiwa watu wazima.
Namna nzuri ya kufundisha upendo, ni kuonyesha upendo, na namna nzuri ya kuonyesha upendo ni kwa matendo.Wanafunzi wanaohitimu kidato cha 6 wakitoa burudani yaoRaha ya kuhitimu Shule..Wanafunzi wanaohitimu Shule hiyo ya Kajumulo Girls High School ya Wasichana wakicheza Ngoma yaoFull kufunguka!!Ngoma kutoka Ngote nayo ilianza kutumbuizaNgoma ikichanganywa vilivyo na Wasanii kutoka kundi la Ngote BukobaMizuka imepanda..Chezea Ngote wewe!Mpaka
Viongozi, Prof. Anna Tibaijuka, Mgeni rasmi Mheshimiwa mgeni rasmi, Bi.
Edwina Lupembe, Mkuu wa Shule nao wakasimama kucheza ngoma hiyo
inayovuma vilivyo hapa Bukoba.Ngoma ilichukua nafasi hapa...Viongozi wakaichambua vilivyo!Unauliza Ngoma Bukoba!!??Prof. Anna Tibaijuka akiikubali ngoma hiyo na kuwapa makofi kwa wingi pamoja na Mgeni Rasmi.Mheshimiwa
mgeni rasmi, Bi. Edwina Lupembe; Mkurugenzi wa “Mkombozi Commercial
Bank” akuishia hapo alitoa Computer kwa Shule hiyo.
Zawadi
ya Computer ikipokelewa na uongozi mzima wa Shule hiyo kutoka kwa
Mheshimiwa mgeni rasmi, Bi. Edwina Lupembe ambaye ni Mkurugenzi wa
“Mkombozi Commercial Bank”.
Uzinduzi wa Jarida la kila mwaka kwa Shule hiyo ulifanta!Zoezi la Kugawa vyeti pia nalo lilifata...Mzazi akipata picha na Mwanae aliyehitimu Mama na Mwana..
No comments:
Post a Comment