Tuesday, March 4, 2014

Mwenyekiti wa Chadema akitabiria CCM ushindi wa kishindo uchaguzi wa Kalenga



Mgombea ubunge Jimbo la Kalemnga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa (kushoto) akijiunga kucheza ngoma ya asili ya kabila la wahehe iliyokuwa ikiongozwa na msanii maarufu wa filamu na muziki, Dokii wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Kalenga leo katika Kijiji cha Kikombwe, Iringa Vijijini. Katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chadema wa Kijiji hicho alikitabiria CCM ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo.
Wafuasi wa CCM katika Kijiji cha Lupembelwasenga wakishangilia kwa furaha walipokuwa wakimlaki mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa kwenye mkutano wa kampeni leo.
Msanii wa filamu na muziki, Dokii akitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni hizo, katika Kijiji cha Lupembelwasenga.
Ofisa wa CCM Makao Makuu ya Umoja wa Vijana, Mwampamba ambaye alijitoa Chadema, akielezea kisa cha kujitoa kwenye chama hicho na kujiunga na CCM.
Mwenyekiti wa Chadema katika Kijiji cha Lupembelwasenga, Ezekiel Kibiki (kushoto), akikabidhi kadi ya chama hicho kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa, Delfina Mtavilalo na kuamua kujiunga na CCM leo, wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Kalenga. Kibiki aliitabiria CCM ushindi katika uchaguzi huo.Pia alisema kuwa tayari amewashawishi wanachama wengine wa chama hicho, kujiunga na CCM.
Wanakijiji cha Lupembelwasenga wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya mgombea uchaguzi wa Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo leo mchana.
Mgombea Ubunge, Godfrey Mgimwa akiwapungia mkono wananchi alipowasili katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kikombwe leo.
Dokii akiungana na wananchi kucheza ngoma ya asili ya kabila la Wahehe katika Kijiji cha Kikombwe.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa, Delfina Mtavilalo, akichuchumaa ikiwa ni heshima ya kumuombea kura mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kijiji cha Kikombwe, Iringa Vijijini leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe akielezea mikakati ya chama hicho, kukigalagaza chama cha Chadema katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga leo mchana katika Kijiji cha Kikombwe, Iringa Vijijini.
Godfrey Mgimwa akijinadi katika mkutano wa kampeni leo katika Kijiji cha Kikombwe. (Picha zote na Kamanda wa Matukio)

No comments:

Post a Comment