Wednesday, June 26, 2013

Tigo Mini Kabaang kufanya Tamasha jijini Mwanza

 Meneja Chapa wa Tigo Tanzania Bw. William Mpinga akiongea na waandishi wa habari kuhusu
 tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litakalofanyika siku ya jumapili hii bure kabisa katika viwanja
 vya  CCM Kirumba jijini Mwanza, kushoto msanii Diamond Platnumz na kulia msanii Madee ambao 
watatoa shoo siku hiyo na wasanii wengine.
 Msanii wa bongo flava Diamond Platnumz akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
 kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili pembeni 
yake Meneja Chapa wa Tigo Tanzania Bw. William Mpinga.
 Msanii Madee akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la 
Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili pembeni yake ni Meneja Chapa wa Tigo
 Tanzania Bw. William Mpinga na Diamond Platnumz .
 Msanii Richie Mavoko akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la 
Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili kulia kwake ni Msanii Madee, meneja wa
 Tigo Bw. William Mpinga na Diamond Platnumz. 
Wasanii Diamond Platinumz, Madee wa Tip Top na Richie Mavoko katika picha ya pamoja na 
Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga. Wasanii wengine watakaokuwepo ni Fid Q,  Ney wa
 Mitego, Roma Mkatoliki, Recho na Kazi Kwanza.



 Msanii Bora wa mwaka Diamond Platnumz, Fid Q na wasanii 
wengine sita wanatarijiwa kupagawisha mashabiki zaidi ya elfu sitini katika tamasha la Tigo Mini 
Kabaang litakayofanyika jijini Mwanza (Rock city) Jumapili hii ya Juni 30.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo, Meneja wa Chapa wa Tigo Bw. William 
Mpinga alisema kwamba lengo la tamasha hilo ni kujenga mahusiano ya karibu na wateja wao kwa 
 kutumia 
sanaa ya muziki kama njia ya kutangaza huduma za Tigo na bidhaa zake za vifurushi kwa wateja 
wengi zaidi.


“Tunaamini kwamba tamasha hili litajenga mazingira mazuri yakufanya kampuni na
 wateja wetu kuelewana zaidi. Mwisho wa siku tunatarajia wateja wetu kujumuika nasi, kupata 
burudani yakutosha na kuelimishwa zaidi kuhusu huduma zetu mbali mbali zenye ubora 
na unafuu kama Mini Kabaang,” alisema Mpinga.

Mini Kabaang inatoa muda wa maongezi wa dakika 20 za bure, 50MB ya kifurushi cha intaneti, 
pamoja na ujumbe mfupi 100 kwa shilingi 475 tu kwa siku.



Mkutano huo wa waandishi wa habari pia ulihudhuriwa na wasanii wakubwa kama Madee wa Tip Top, 
Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Richi Mavoko, Recho, Kazi Kwanza, Diamond Platnumz na Fid Q, 
ambao ndio wasanii wa Bongo Fleva watakaopamba siku hiyo ya Jumamosi katika viwanja vya CCM 
Kirumba kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni.

“Mimi pamoja na wasanii wenzangu tunayo furaha kubwa kushiriki katika tamasha la Tigo Mini Kabaang 
litakalofanyika jijini Mwanza, hakika watu wa Rock city ni washabiki wakubwa wa muziki wetu, 
na tunatarajia kwenda kuwapa burudani ya kutosha,” alieleza Diamond Platnumz alipoulizwa kuhusu
 tamasha hilo.



“Binafsi nina furaha yakipekee kufanya tamasha langu la kwanza la wazi jijini Mwanza. 
Naamini hao mashabiki elfu sitini na zaidi wataonyesha  mapenzi ya dhati kwa muziki wangu.
 Ninahamu sana ya kufika na kufanya tamasha hii,” aliongeza super staa huyo.



“Tamasha hili la Tigo Mwanza Mini Kabaang pia litawapa fursa mashabiki kujishindia zawadi mbali mbali
kama vile simu, vocha, fulana za nembo ya Tigo na nyingine nyingi. Hakutakuwa na kiingilio siku
hiyo, tunapenda kuwakaribisha kila mteja wa Tigo na mshabiki wa bongo fleva kujumuika na
 kushiriki nasi,” aliongezea Mpinga.



“MINI KABAANG” ni kifurushi cha siku ambacho mteja akijiunga anapata dakika 20 za muda
 wa maongezi ambazo anaweza kuzitumia kupiga simu kwenda mtandao wowote ule, pia anapata
 kifurushi cha 50MB ya intaneti na kuweza kutuma ujumbe mfupi 100 kwa mtandao wowote. 
Kutumia kifurushi hiki mteja anabidi apige namba *148*01#. Huduma hii inapatikana kwa 
wateja wote wa Tigo kwa gharama nafuu ya shilingi 475 tu kwa siku.



Tamasha za Mini Kabaang ni mfululizo wa maonyesho ya muziki yanayoandaliwa na Tigo, 
yamekwisha fanyika Morogoro, Moshi na sasa Mwanza. Mikoa mengine itakayofuata ni Mbeya,
 Dodoma na mikoa mingine.

No comments:

Post a Comment