Katika Viwanja vya Soweto leo kabla ya Mabomu na Risasi |
LEO ARUSHA |
kiukweli Tanzania inapoelekea ni pabaya kwani leo hii kinachoendelea Arusha huwezi amini kama ni Polisi wanaoyafanya yote haya kwa raia wao ambnao wanawategemea kwa ulinzi wao na malizao.
yametokea machafuko ya Amani yaliyopelekea watu kuvunjika Miguu na Mikono huku kukuiwa na fununu kuwa kuna watu wamepoteza Maisha japo haijajulikana kuwa ni kweli au vipi na ni Baada ya Polisi kuwapiga mabomu ya Machozi wananchi wa Chama Cha CHADEMA kwa kushindwa kuelewana baina ya Serikali Jijini Arusha ambayo inalimiliki jeshi ambao wametokea kutokuelewana baina yao na Chadema kutokana na kile kinachodaiwa kuwa Chadema waliomba kibali kufanya Mkutano katika uwanja wa Soweto Arusha kwa ajili ya Kuwaaga Marehemu wao waliopoteza maisha juzi kwenye Mkutano wao ambao pia ulifanyika katika uwanja huo huo na mwishowe Wamiliki wa uwanja huo ambao ni AICC kukataa uwanja wao usitumike katika shughuli hiyo.
Kilichoendelea ni Polisi kuwaamuru wafuasi wa Chadema kuondoka uwanjani hapo kitu ambacho wafuasi wa Chadema Walisusia na mwishowe Polisi wakaanza Kufyatua Mabomu na kuwakimbiza Wafuasi hao kama Mbwa na ndipo kwa kila mtu kutetea roho yake watu waliangukiana na kukanyagana kitendo ambacho hadi sasa wengi ni walemavu na wameupata ulemavu huo leo.
Inaniuma zaidi kuwa Kuna Waandishi Watano leo wameumia Vibaya akiwepo Nickson Robert na Irene wa MJ Radio.
hata hivyo Kauli ya kamanda Mkuu wa Jeshi la Polisi amesema bado hajafanya Uchunguzi wa Kina kuhusu Watu Kupoteza Maisha au kuumia kutokana na Ghasia hizo ila kikubwa amesema Wanawashikilia Wabunge wawili wa CHADEMA ambao ni Tundu Lisu na Mbunge wa Mbulu Mh. Akonai kwa mahojiano maalum kuhusiana na Tukio zima la Leo.
mh; Tundu Lisu |
Aidha jeshi la Polisi Arusha limesema linawashikilia watu watatu Wanaodhaniwa kuhusika na Ulipuaji wa Bomu Juzi Viwanja vya Soweto Arusha na kupelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine zaidi ya 70 kuumizwa vibaya..
No comments:
Post a Comment